Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mfumo wa PlanRep Kurahisisha Utendaji Kazi Serikalini
Aug 29, 2017
Na Msemaji Mkuu

Na Beatrice Lyimo

Mfumo wa kielektroniki(PlanRep) ulioboreshwa wa kuandaa Mipango, Bajeti na Ripoti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa utarahisisha utendaji kazi katika maeneo ya uandaaji wa Mipango, bajeti na ripoti mbalimbali

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kuhusiana na mafunzo hayo Katibu wa Afya Bi. Stella Mwakikunga kutoka Manispaa ya Ilemela amesema kuwa mfumo huo utarahisisha utendaji kazi hasa katika maeneo ya uandaaji wa Mipango, Bajeti na Ripoti mbalimbali zinazohusu Halmashauri husika.

Bi. stella ameongeza kuwa mbali na kurahisisha utendaji kazi pia mfumo huo utakuwa wazi hasa kwa baadhi ya watumishi wanaodanganya kuhusu shughuli mbalimbali kwa wananchi.

Aidha Bi.Stella ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kuwasilisha ukomo wa bajeti mapema ili kuweza kurahisisha utumiaji wa mfumo kwani mfumo huo huenda kwa muda.

Kwa upande wake Kaimu Mwekahazina wa  Halmashauri ya Hanang Mkoa wa Manyara Bwn.Joseph Allay amesema kuwa mfumo huo utasaidia kupunguza gharama kwa Serikali kwani awali zoezi la uaandaaji wa bajeti lilichukua muda mrefu ambapo huwalazimu watumishi kuwa mbali na kituo cha kazi.

"Mfumo utasaidia kurahisisha utendaji kazi ambapo utawezesha kila maeneo ya maamuzi kufanyika katika kituo husika na hivyo kutokuwa na malalamiko kama ilivyokuwa awali" aliongeza Bwn. Allay.

Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma(PS3 ) ni mradi wa miaka mitano ukiwa na lengo la kuboresha utoaji wa huduma za Serikali za Mitaa kwa jamii hasa zile zenye uhitaji zaidi

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi