[caption id="attachment_1748" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akipokelewa na wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam alipokuwa katika ziara ya kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC).Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Sipora Liana na Mstahiki Meya wa Jiji hilo Isaya Mwita.[/caption] Nuru Juma Serikali imeipongeza Bodi na Menejimenti nzima ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) kwa juhudi zao zakurejesha uhai wa Shirika hilo richa ya changamoto wanazo kumbana nazo. Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –TAMISEMI), George Simbachawene wakati akipokea taarifa fupi ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) na Shirika la Masoko Kariakoo alipokutana na menejinti ya mashirika hayo leo. Waziri Simbachawene alisema kuwa amepitia taarifa ya Shirika hilo na kuridhika nayo hivyo hana budi kuipongeza timu nzima ya uongozi kwani kwa muda mfupi imeweza kufanya mabadiliko na kuweza kuliinua tena Shirika hilo. “Pamoja na kuipongeza bodi hii lakini napenda kuwashauri kuangalia maeneo mengine ya kuwekeza kama kufungua maeneo mengi zaidi ya burudani kwani hilo ndilo lilikuwa lengo la kuanzishwa kwa DDC,ikiwa ni pamoja na kuweka mahali ambapo watoto wataweza kucheza ili kuhakikisha shirika linajiongezea kipato na kuiongezea Serikali kipato pia,” alisema Waziri Simbachawene. Simbachawene alitumia nafasi hiyo kuwaagiza Wakuu wa Mashirika ya Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanaandaa taarifa nyingine itakayohusisha mali zote za mashirika hayo. [caption id="attachment_1750" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akizungumza na menejimenti za Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) wakati wa ziara yake katika ofisi za mashirika hayo leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo Dkt. Hoseana Bohela Lunogelo.[/caption] [caption id="attachment_1751" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Sipora Liana akifafanua jambo wa mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (mbele) alipokuwa katika ziara ya kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.[/caption] Aidha ameutaka uongozi wa Shirika la Masoko Kariakoo kuwa wabunifu kwa kuanzisha masoko sehemu mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni mkakati wa kusogeza huduma kwa wananchi na njia ya kuongeza ajira kwa vijana. Alilitaka Shirika hilo kuachana na mawazo ya kizamani na badala yake wajipange kimkakati ili kuendana na wakati ikiwemo kufikiria namna ya kuwaza kushusha mizigo katika soko hilo kwani serikali haitaweza kuruhusu maroli ya mizigo kufika katika soko hilo ili kupunguza ya kuepuka msongamano katikati ya jiji. Aliushauri uongozi huo uandae mikakati ya kuwezesha soko hilo kuwa la kiwango cha juu (Super Market) na kuwalipisha wafanyabiashara kiwango kinachoendana na bei halisi ya soko kama ambavyo wapangishaji wengine wamekuwa wakitoza ili kukuza kipato kwa Taifa. [caption id="attachment_1752" align="aligncenter" width="750"] Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akisisitiza jambo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (kulia) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo katika Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo Dkt. Hoseana Bohela Lunogelo.[/caption] [caption id="attachment_1753" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo Dkt. Hoseana Bohela Lunogelo akielezea jambo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (kulia) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo katika Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo. Katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita.[/caption] [caption id="attachment_1756" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam(DDC) wakifuatilia maelekezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni(hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi katika Mashirika ya Masoko Kariakoo na Shirika la Maenedeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC).[/caption] Waziri Simbachawene ameahidi kushirikiana na mashirika hayo katika kutatua changamoto ambazo zinahitaji msaada wa uongozi na kuwataka wafanye kazi kwa bidii kwani Serikali ya Awamu ya Tano inahitaji watu wanaojituma na kuchapa kazi. Awali akiwasilisha taarifa fupi ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam Meneja Mkuu wa Shirika hilo Rwandiko Manumbu alisema kuwa pamoja na changamoto wanazokumbana nazo Shirika limefanikiwa kutoa shilingi milioni 140/- kama gawio kwa mwanahisa wake ambaye ni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. “Mhe. Waziri, kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Shirika hili tumeweza kutoa gawio la kiasi cha shilingi milioni 140/- kwa Halmashauri ya Jiji na haya ni mafanikio makubwa kwetu,” alisema Manumbu. [caption id="attachment_1757" align="aligncenter" width="750"] Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko la Kariakoo Hetson Msalale Kipsi akiwasilisha taarifa fupi ya Shirika hilo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (hayupo pichani) wakati wa ziara ya yake kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.[/caption] [caption id="attachment_1762" align="aligncenter" width="750"] Meneja Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC), Rwandiko Manumbu akiwasilisha taarifa fupi ya Shirika hilo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (kulia) wakati wa ziara ya yake kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.Katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_1765" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akipokelewa na baadhii ya wajumbe wa Bodi za Mashirika ya Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) NA Shirika la Masoko Kariako alipowasili katika Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.[/caption] [caption id="attachment_1766" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akisalimiana na mmoja wa wafanyabiashara katika Soko la Kariakoo Shimoni wakati wa ziara ya kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.[/caption] [caption id="attachment_1767" align="aligncenter" width="750"] Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita (kushoto) akimuongoza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni(mwenye suti nyeusi) kuelekea katika Ofisi za Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) wakati wa ziara ya kikazi kutembelea Shirika hilo pamoja na Shirika la Masoko Kariakoo leo Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_1771" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akizungumza na wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama Machinga wanaopanga bidhaa zao mbele ya Ofisi za Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi kutembelea Shirika hilo pamoja na Shirika la Masoko Kariakoo leo Jijini Dar es Salaam. (Picha zote: Frank Shija) [/caption] Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amempongeza Waziri Simbachawene kwa utayari wake wa kushughulikia changamoto zinazo yakabli mashirika hayo ikiwa ni pamoja na kutenga muda wake kuja kusikiliza matatizo yao. Pamoja na pongezi hizo Mwita alishauri Shirika la Maendeleo la Dar es Salaam (DDC) kuangalia uwezekano wa kurejesha bendi za muziki kama ambavyo Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alivyokuwa amedhamiria wakati wa uanzishwaji wa Shirika hili. Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) na Shirika la Masoko Kariakoo ni mashirika ya Umma yanayoongozwa na Serikali kupitia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam chini ya Sheria za Makampuni namba 2012 ya mwaka 1971 na Sheria ya Bunge namba 36 ya mwaka 1974, “The Kariakoo Market Corporation Act, 1974”