Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mdaiwa Sugu Jiji la Arusha Anaswa
Sep 18, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr. Maulid Suleiman Madeni akiwa ndani ya duka la mmoja wa wafanyabiashara wa stendi dogo ya Jiji la Arusha akikagua leseni ya biashara pamoja na risiti za ushuru wa kibanda.[/caption]  
[caption id="attachment_35349" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr. Maulid Suleiman Madeni (wa kushoto) alipokuwa akifanya operesheni ya kukusanya mapato ya jiji la arusha.[/caption]  
Na. Fatuma S. Ibrahimu – Arusha Jiji 
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr. Maulid Suleiman Madeni  amemnasa mfanyabishara Bw. Mouris Makoi na kumfungia vibanda 69 kutokana na kudaiwa ushuru wa shilingi milioni 85.
Hatua ni katika muendelezo wa operesheni ya ukusanyaji wa mapato inayofanywa na Dkt. Madeni ambapo amefungia vibanda  zaidi ya vibanda 90 vikiwemo vya Bw. Makoi katika stendi ndogo Jijini Arusha kwa kuwa na malimbikizo ya madeni na kukwepa ushuru wa vibanda hivyo pamoja na kutokuwa na leseni za biashara .
Dr. madeni amesema kuwa Bw. Makoi ni mdaiwa sugu na amekuwa akikwepa kulipa kodi ya Serikali kwa mda mrefu kitendo kinachopelekea kuinyima mapato Halmashauri na ameagiza alipe deni lote ama ajisalimishe ofisini kwake kabla hatua nyingine za kisheria hazijachukuliwa dhidi yake .
Pia Dr. Madeni amesikitishwa na baadhi wafanyabiashara wanaojificha chini ya miamvuli ya vyama vya siasa ili kukwepa kulipa kodi ya Serikali na kuwaasa wawe mfano bora katika kuhamasisha zoezi la ulipaji kodi.
“Kuna wafanyabiashara wanajificha kwenye vyama Fulani ili kukwepa kulipa kodi ya Serikali, nawaasa kuacha mara moja mazoea hayo kwani Serikali ya awamu hii imejikita katika kuwaletea wananchi maendeleo bila kujali dini, kabila wala itikadi za vyama” alisema Dr. Madeni
“Pia kuna wenye mikataba ya Halmashauri lakini wamepangisha watu wengine na kuwachajisha kodi ya juu kinyume na sheria  kwa mfano  kuna baadhi ya vibanda vinapaswa kulipiwa laki moja lakini wenye mikataba wanachukua laki mbili mpaka tatu kwa wapangaji wao kitu ambacho ni unyonyaji na ukatili wa hali ya juu hivyo nimeamuru wafutiwe mikataba yao na wapewe wapangaji ili wawe wanalipa ushuru moja kwa moja katika Halmashauri” aliongeza Mkurugenzi huyo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi