Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mchambuzi Amsifu Mwalimu Nyerere, Rais Ruto Akitembelea Tanzania
Oct 10, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Ahmed Sagaff, MAELEZO

Mchambuzi wa Diplomasia amemsifu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuasisi mahusiano baina ya Tanzania na Kenya ikiwa siku chache zimesalia kuelekea kumbukizi ya miaka 23 ya kifo cha Baba wa Taifa.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na chaneli ya televisheni ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Mchambuzi Abdulkarim Atiki amesema kitendo cha Mwalimu Nyerere kuwapokea na kuwahifadhi wapigania uhuru kutoka Kenya ndio asili.

“Hata mpigania uhuru wa Kenya kiongozi wa Maumau, Ndg. Dedan Kimathi wakati alipokuwa akitafutwa na wakoloni nchini Kenya, alikuja kukimbilia Tanzania, alikaa Tanga.

“Watanzania walimuhifadhi, wapiganaji wengi wa Maumau walikuja kujihifadhi huku Tanganyika (sasa Tanzania), kwa hiyo udugu wa nchi zetu sisi ni wa damu kabisa”, ameeleza Ndg. Atiki.

Ikumbukwe kuwa mara baada ya Tanzania Bara kupata uhuru mwaka 1961, Mwalimu Nyerere akaongoza mapambano ya ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika kwa kuasisi Umoja wa Nchi za Mstari wa Mbele (Frontline Satates), hivyo kuyasaidia mataifa ya kusini kupata uhuru wake.

Vilevile, Mwalimu Nyerere aliongoza harakati za kupigania umoja wa Bara la Afrika pamoja na kutatua migogoro kwenye mataifa mbalimbali ya bara hili huku Tanzania ikishiriki katika operesheni mbalimbali za kulinda amani Darfur, DRC, Lebanon na kwingineko. 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi