Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Chaneli ya Utalii Kuzinduliwa Disemba Mwaka Huu
Oct 16, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_36859" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Susan Mlawi akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kamati inayoshughulikia uanzishwaji wa Chaneli ya Runinga ya Utalii leo jijini Dodoma. Chaneli hiyo inaanzishwa kufuatia agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipotembelea studio za Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) mnamo tarehe 16, Mei, 2017. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda.[/caption]

Na Jacquiline Mrisho

Serikali imeazimia kuzindua Chaneli ya Utalii inayotegemewa  kurushwa kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) mnamo mwezi Disemba mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Susan Mlawi wakati wa Kikao cha Kamati inayofuatilia uanzishwaji wa chaneli hiyo.

Bi. Susan amesema kuwa vikao vya wadau na wataalam mbalimbali vitakavyowezesha uanzishwaji wa chaneli hiyo vinaendelea ambapo katika kikao hicho imetolewa taarifa ya hatua zilizofikiwa ambazo zimeonekana kuleta mafanikio makubwa.

[caption id="attachment_36860" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kamati inayoshughulikia uanzishwaji wa Chaneli ya Runinga ya  Utalii leo jijini Dodoma. Chaneli hiyo inaanzishwa kufuatia agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipotembelea studio za Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) mnamo tarehe 16, Mei, 2017. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Susan Mlawi.[/caption]

"Tumekusudia kuifanya chaneli hii ambayo tunatarajia uzinduzi wake utafanyika mwezi Disemba mwaka huu kuwa na vipindi bora vyenye kugusa utalii wa kila aina. Aidha, tunategemea kuweka lugha mbalimbali ambazo zitasaidia watu wengi kutoka mataifa mbalimbali kuweza kuitazama."

Ameongeza kusema kuwa hadi kufikia muda huu tayari fedha za mitambo itakayoweza kuanzisha chaneli hiyo zimeshapatikana na ametoa rai kwa TBC kutoa kipaumbele katika maandalizi ya chaneli hiyo na kuandaa utaratibu maalum wa kusimamia matangazo yake.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa ni muhimu chaneli hiyo ionekane sehemu mbalimbali duniani ili kupata wadau wengi watakaoweza kuweka matangazo yao na kuiwezesha chaneli hiyo kujiendesha.

[caption id="attachment_36861" align="aligncenter" width="750"] Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki akielezea jambo wakati wa kikao cha kamati inayoshughulikia uanzishwaji wa Chaneli ya Runinga ya Utalii leo jijini Dodoma. Chaneli hiyo inaanzishwa kufuatia agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipotembelea studio za Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) mnamo tarehe 16, Mei, 2017. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi. Susan Mlawi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda.[/caption]

Amefafanua kuwa matangazo kupitia chaneli hiyo itakayotangaza utalii wa Tanzania yataingiza fedha nyingi ambazo zitasaidia kujiendesha badala ya nchi kutumia fedha nyingi kuutangaza utalii nje ya nchi.

"Kupitia chaneli hii, tunataka utalii uchukue sura mpya katika kuvutia uwekezaji kwani itawezesha Tanzania kujitangaza kiutalii katika nchi mbalimbali duniani na kuongeza Pato la Taifa," alisema Prof. adolf Mkenda.

Naye Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania,  Bi. Joyce Fissoo amesema, nchi ikiwa na chaneli yenye maudhui ya utalii itasaidia Watanzania kufahamu kwa urahisi vivutio vilivyopo nchini pia itawafanya wadau mbalimbali kufahamu sio tu utalii bali pia masuala ya kiutamaduni.

[caption id="attachment_36862" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayoub Ryoba akielezea hatua zilizofikiwa za uanzishwaji wa Chaneli ya Runinga ya Utalii wakati wa kikao cha kamati inayoshughulikia uanzishwaji wa chaneli hiyo leo jijini Dodoma. Chaneli hiyo inaanzishwa kufuatia agizo la Rais, Dkt. John Pombe Magufuli alipotembelea studio za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) mnamo tarehe 16, Mei, 2017. Kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bibi. Joyce Fissoo na Mwenyekiti wa Kamati ya Uanzishwaji wa Chaneli hiyo, Gabriel Nderumaki.[/caption] [caption id="attachment_36863" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bibi. Joyce Fissoo akielezea jambo wakati wa kikao cha kamati inayoshughulikia uanzishwaji wa Chaneli ya Runinga ya Utalii leo jijini Dodoma. Chaneli hiyo inaanzishwa kufuatia agizo la Rais, Dkt. John Pombe Magufuli alipotembelea studio za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) mnamo tarehe 16, Mei, 2017. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Susan Mlawi, Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayoub Ryoba, Mwenyekiti wa Kamati ya hiyo, Gabriel Nderumaki.[/caption] [caption id="attachment_36864" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya washiriki wa kikao cha kamati inayoshughulikia uanzishwaji wa Chaneli ya Runinga ya Utalii wakifuatilia kikao baina ya kamati hiyo na Makatibu Wakuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Susan Mlawi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda (hawapo pichani) leo jijini Dodoma. Chaneli hiyo inaanzishwa kufuatia agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipotembelea studio za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) mnamo tarehe 16, Mei, 2017. (Picha na: Idara ya Habari).[/caption]

Vile vile chaneli hii itawawezesha wadau kufahamu maeneo mahususi ya upigaji picha za mnato na jongefu ambazo zitaifanya nchi kujulikana zaidi nje ya nchi kupitia picha.

Uanzishwaji wa chaneli ya utalii kupitia TBC ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa wakati alipotembelea shirika hilo mnamo mwaka 2017.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi