Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mazingira Mazuri ya Uwekezaji Yachagiza Ukuaji NSSF - Prof. Ndalichako
Aug 17, 2023
Mazingira Mazuri ya Uwekezaji Yachagiza Ukuaji NSSF - Prof. Ndalichako
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa mwaka 2022/23 kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii tarehe 17 Agosti, 2023 bungeni jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi.
Na Mwandishi Wetu - Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyowekwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa sekta binafsi yamechochea ukuaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Aidha, Mhe. Ndalichako amesema ukuaji huo umepelekea thamani ya mfuko kuongezeka pamoja na michango ya wanachama.

Baadhi ya Wajumbe Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, wakifuatilia kwa makini maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), bungeni, tarehe 17 Agosti, 2023, jijini Dodoma.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo Agosti 17, 2023 alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya NSSF kwa mwaka 2022/23 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi wa Maendeleo ya Jamii.

Amesema kwa mwaka 2022, Mfuko huo uliandikisha wanachama 233,644 hadi kufikia Juni, mwaka 2023 kulikuwa na wanachama 243,895 na matarajio ifikapo Juni 2024 ni kuwa na wanachama 277,279.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Mendeleo ya Jamii, Mhe. Fatuma Toufiq (kushoto) akizungumza jambo mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), leo tarehe 17 Agosti, 2023 bungeni jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa kamati, hiyo Bi. Aziza Kheir.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akifafanua jambo kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, bungeni, tarehe 17 Agosti, 2023, jijini Dodoma.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq, ameutaka Mfuko wa NSSF kuhakikisha unaongeza wanachama zaidi hasa waliopo kwenye sekta isiyo rasmi.

Akijibu hoja za Wabunge, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, amewahakikishia Wabunge kuwa atazingatia maoni yao ili kuendelea kuboresha huduma kwa wanachama wake.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi