Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matumizi ya Teknolojia Mbadala Yapunguza Gharama za Ujenzi wa Barabara kwa 50%
Aug 24, 2023
Matumizi ya Teknolojia Mbadala Yapunguza Gharama za Ujenzi wa Barabara kwa 50%
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wakala hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 jijini Dodoma kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Agosti 24, 2023.
Na Na Mwandishi Wetu

Matumizi ya Teknolojia mbadala na malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi kwa ajili ya ujenzi wa barabara na madaraja imeweza kupunguza gharama zaidi ya 50%.

Hayo yameelezwa leo na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff  wakati akiongea na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari - MAELZO jijini Dodoma.

“TARURA imeweka kipaumbele cha kutumia malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi ili kupata ufanisi wa gharama za ujenzi.

Mhandisi Seff amesema  hadi kufikia mwezi Machi,2023, TARURA  imejenga madaraja 163 ya mawe yenye thamani ya bilioni 8.7 ambapo gharama imepungua.

Ametaja mikoa iliyojengwa madaraja hayo kuwa ni Kigoma (92), Singida (24), Tabora (5), Kilimanjaro (10), Mbeya (2), Arusha (6), Morogoro (2),  Rukwa (3), Pwani (1), Ruvuma (3) pamoja na Iringa (15).

Aidha, amesema bado wanaendelea kufanya majaribio ya teknolojia mbalimbali ili kutumia udongo uliopo eneo la kazi badala ya kusomba kutoka maeneo mengine ya mbali.

“Teknolojia hizo ni pamoja na Ecoroads, Ecozyme na GeoPolymer ambao hadi sasa kwa kutumia teknolojia ya Ecoroads katika Jiji la Dodoma imejengwa Kilomita moja (1) ambayo imekamilika na katika Wilaya ya Mufindi zitajengwa Kilomita kumi (10)”.Aliongeza

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi