Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio kuhusu maandalizi ya ujenzi wa mradi wa LNG (mradi wa kusindika gesi kuwa kimiminika ) katika eneo Likong’o Manispaa ya Lindi wakati alipotembelea eneo hilo akiwa katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani Lindi, Oktoba 5, 2021. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Hajat Zainab Telack.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama michoro ya ujenzi wa mradi wa maji wa Mitwero, Mkwaya na Kitunda wilayani Lindi, Oktoba 5, 2021
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Mnara iliyopo Rondo katika Jimbo la Mtama Mkoani Lindi, Oktoba 5, 2021.
Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Benard Membe (katikati), Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Lindi, Athumani Seif (kulia) na Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Naaz Mangochi wakifurahia hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza na wananchi katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Mnara katika jimbo la Mtama, Mkoa wa Lindi, Oktoba 5, 2021
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Mhashamu Bruno Ngonyani wakati alipotembelea hospitali ya Nyangao katika Jimbo la Mtama, Oktoba 5, 2021.