Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio Katika Picha; Tamasha la Wanawake Wajasiriamali Jijini Dodoma
Oct 20, 2018
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_37131" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Roida Andusamile akisisitiza kuhusu hatua iliyochukuliwa na Serikali katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo kupata alama ya ubora wa bidhaa wanazozalisha ili kuchochea ujenzi wa uchumi wa Viwanda ambapo Serikali inalipa gharama hizo kwa wajasiriamali wadogo, hayo ilikuwa wakati wa Tamasha la Mwanamke Mjasiriamali linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wajasiriamali wa hapa nchini na kutoka nchini Burundi.[/caption] [caption id="attachment_37132" align="alignnone" width="900"] Afisa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kati Bw. Sileja Lushibika akieleza hatua zinazopaswa kufuatwa na mjasirimali ili kupata alama ya ubora kwa mmoja wa wananchi waliofika katika Banda la Shirika hilo wakati wa Tamasha la Mwanamke Mjasiriamali linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wajasiriamali wa hapa nchini na kutoka nchini Burundi.[/caption] [caption id="attachment_37133" align="aligncenter" width="900"] Afisa Elimu, Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bw. Paulus Oluochi akizungumzia umuhimu wa kuzingatia vipimo kwa wajasirimali wakati wa kufungasha na kuzalisha bidhaa mbalimbali ili kuchochea dhana ya ujenzi wa uchumi wa Viwanda,hiyo ilikuwa wakati wa Tamasha la Mwanamke Mjasiriamali linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wajasiriamali wa hapa nchini na kutoka nchini Burundi.[/caption] [caption id="attachment_37134" align="aligncenter" width="900"] Afisa Elimu, Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bw. Paulus Oluochi akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa katika kuhakikisha kuwa wajasiriamali wote wanafikiwa na huduma za Wakala huo ili kutekeleza kwa vitendo matwakwa ya sheria ya vipimo na kanuni zake.[/caption] [caption id="attachment_37135" align="aligncenter" width="900"] Afisa Vipimo wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) Bi. Zaidat Gharibu akionesha jinsi wanavyohakiki vipimo mbalimbali ikiwemo upimaji wa gesi yakupikia majumbani.[/caption]

(Picha zote na Frank  Mvungi)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi