Matukio katika Picha: Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi Azungumza na Maafisa kutoka Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania.
Oct 09, 2023
Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi akizungumza na Maafisa kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania. Mazungumzo ya kikao hicho yamelenga kuimarisha mashirikiano baina ya Ubalozi wa Marekani na Serikali hususan Idara ya Habari, kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Idara ya Habari- MAELEZO Jijini Dar es Salaam.
Na
Paschal Dotto -MAELEZO