Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio Katika Picha Bungeni Leo Septemba 6
Sep 06, 2018
Na Msemaji Mkuu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Geogre Mkuchika akieleza umuhimu wa muswaada wa Sheria ya Bodi ya Taaluma ya Walimu Tanzania, 2018. (The Tanzania Teachers Professional Board Act, 2018) wakati wa kupitishwa kwa muswaada huo leo Bungeni Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa  Sima akieleza mikakati ya Serikali kuhakikisha inatunza mazingira ya ziwa manyara ili kuondoa athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisisitiza jambo wakati akijibu hoja za wabunge leo Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kupitisha muswaada wa Sheria ya Bodi ya Taaluma ya Walimu Tanzania, 2018. (The Tanzania Teachers Professional Board Act, 2018).

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso akisisitiza mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa wananchi wote wanafikiwa na huduma ya maji safi na salama kote nchini.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi waliokuwa na akaunti katika iliyokuwa  Benki ya FBME  wanalipwa haki zao kwa mujibu wa sheria na Kanuni za utumishi baada ya Benki hiyo kufungwa.

 Sehemu ya wageni waliofika Bungeni  kama wanavyoonekana katika picha leo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Rita Kabati akisisitiza kuhusu umuhimu wa wananchi kupata huduma bora za maji safi na salama wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Mussa Zungu akisisitiza jambo wakati wa kupitishwa kwa muswaada wa Sheria ya Bodi ya Taaluma ya Walimu Tanzania, 2018.(The Tanzania Teachers Professional Board Act, 2018) leo Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima, leo Bungeni Jijini Dodoma.Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula akieleza hatua zilizochukuliwa na Serikali kuondoa mgogoro kati ya wananchi na Manispaa ya Mtwara Mikindani unaotokana na eneo la Mjimwema na Tangira lililopimwa kwa ubia kati ya Manispaa na Taasisi ya UTT-PID mwaka 2003.

(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi