Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio Katika Picha Bungeni Leo Aprili 24, 2019
Apr 24, 2019
Na Msemaji Mkuu

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, mhandisi Hammad Masauni, akisisitiza kuhusu askari wa kikosi cha usalama barabarani kuzingatia sheria kanuni na taratibu wanapotekeleza majukumu yao  leo  Bungeni Jijini Dodoma. [caption id="attachment_42355" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola  akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake leo bungeni Jijini Dodoma.[/caption]

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola, akisisitiza jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) leo Bungeni Jijini Dodoma.

Naibu Waziri Wizara ya Nishati, Mhe. Subira Mgalu, akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali katika kuhakikisha kuwa gesi inawafikia wazalishaji  katika viwanda vyote vilivyopo katika ukanda unaopitiwa na bomba hilo kati ya Mtwara na Dar es Salaam kulingana na maombi ya kuunganishiwa huduma hiyo.

Wanafunzi wa shule ya msingi Mzakwe ya Jijini Dodoma wakiwa mbele ya ukumbi wa Bunge leo Jijini Dodoma mara baada ya kukamilisha ziara ya mafunzo Bungeni leo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola akisisitiza jambo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

Katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu,(wakwanza kushoto) akifuatilia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi wakati Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola akiwasilisha hotuba hiyo leo Bungeni  Jijini Dodoma.

Naibu Waziri Wizara ya Nishati, Mhe. Subira Mgalu  akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali katika kuhakikisha kuwa gesi inawafikia wazalishaji  katika viwanda vyote vilivyopo katika ukanda unaopitiwa na bomba hilo kati ya Mtwara na Dar es Salaam kulingana na maombi ya kuunganishiwa huduma hiyo.

(Picha zote na Frank Mvungi)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi