Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio Katika Picha Bungeni Leo
Nov 09, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_37965" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Kangi Lugola akitoa ufafanuzi wa taarifa zilizosambaa mitandaoni kuhusu ushoga. Kwenye ufafanuzi wake Waziri Lugola ameliambia bunge Serikali haitaruhusu wananchi kuvunja sheria kwa kufanya vitendo kinyume na uumbaji uliokusudiwa na Mungu.[/caption] [caption id="attachment_37963" align="aligncenter" width="819"] Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe bungeni leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu. Kwenye majibu yake Prof. Kabudi amelieleza bunge serikali haiwezi kutoa ufafanuzi kama alivyotaka mheshimiwa Zitto kwani kufanya hivyo kutaathiri mwenendo wa mashauri ya madai yanayoendelea kwenye mahakama mbalimbali za kimataifa.[/caption] [caption id="attachment_37962" align="aligncenter" width="758"] Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, akisisitiza kuhusu mikakati mbalimbali ya Serikali kuhakikisha asilimia 90 ya wananchi wa maeneo ya mjini na asilimia 85 ya wananchi wa vijijini wanapata huduma ya maji safi na salama ifikapo mwaka 2020.[/caption]

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, akibadilishana mawazo na  Waziri wa Madini  Mhe. Angellah  Kairuki na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Anthony Mavunde leo  Bungeni  Jijini  Doodma wakati wa kipindi cha maswali na  majibu.

Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Elias Kuandikwa, akieleza mikakati ya Serikali kujenga daraja jipya la mto Wami. Kwa mujibu wa maelezo ya Mhe. Kuandikwa ujenzi wa daraja hilo jipya umeshaanza na utachukua muda wa miezi 24 kukamilika.

[caption id="attachment_37961" align="aligncenter" width="900"] aibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa akifurahia jambo na mtawa wa Shirika la Maria Imaculata na ujumbe wake walipomtembelea Bungeni leo Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_37967" align="aligncenter" width="900"] Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Shirika la Maria Immaculata walipomtembelea Bungeni leo Jijini Dodoma.[/caption]  

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi