Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza kikao cha tano cha mkutano wa kumi na mbili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.Kapt Mstaafu George Mkuchika akilieleza Bunge kuwa Serikali imeshatoa kibali cha kuajiri watumishi wapya 15000 ili kuziba pengo lilisababishwa na kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti leo Bungeni Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt Faustine Ndugulile akielezea mpango mkakati uliowekwa na Serikali ili kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ikiwemo kupitia kamati za ulinzi zilizowekwa wakati wa kikao cha tano mkutano wa kumi na mbili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe akieleza faida za kupatikana kwa Sera mpya ya Maendeleo ya Michezo leo Bungeni Jijini Dodoma, ambapo amesema uratibu wa rasimu kamili ya sera hiyo umefikia hatua za mwisho na Wizara yake itakamilisha zoezi hilo ndaniya muda mfupi ujao.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Omary Mgumba akieleza tozo mbalimbali zilizotolewa na Serikali katika zao la kahawa ambapo imesaidia kuimarisha bei ya kahawa nchini wakati wa kikao cha tano mkutano wa kumi na mbili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu akieleza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kuboresha huduma ya umeme nchini wakati wa kikao cha tano mkutano wa kumi na mbili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea Jijini Dodoma.