Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio Katika Picha Bungeni Leo
Jun 20, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_33058" align="aligncenter" width="831"] Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akizungumza wakati wa kikao cha majadiliano ya hoja za Mapendekezo ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2018/19, Hali ya Uchumi wa Taifa na Mpango wa Maendeleo wa Taifa leo Bungeni Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_33059" align="aligncenter" width="768"] Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akijibu hoja wakati kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_33060" align="aligncenter" width="634"] Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akitoa ufafanuzi kuhusu tukio la maafisa wa Wizara yake kufanya ukaguzi katika mgahawa wa Bunge bila idhini ya Bunge wakati kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_33061" align="aligncenter" width="1000"] Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Joseph Kakunda wakati wa kikao cha majadiliano ya hoja za Mapendekezo ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2018/19, Hali ya Uchumi wa Taifa na Mpango wa Maendeleo wa Taifa leo Bungeni Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_33062" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu Mhe. Jenista Muhagama akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dokta Adelardus Kilangi wakati wa kikao cha majadiliano ya hoja za Mapendekezo ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2018/19, Hali ya Uchumi wa Taifa na Mpango wa Maendeleo wa Taifa leo Bungeni Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_33063" align="aligncenter" width="768"] Mbunge wa Jimbo la Kibakwe wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma, Mhe. George Boniphace Simbachawene akichangia hoja wakati wa kikao cha majadiliano ya hoja za Mapendekezo ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2018/19, Hali ya Uchumi wa Taifa na Mpango wa Maendeleo wa Taifa leo Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Anastazia James Wambura.[/caption] [caption id="attachment_33064" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu, Mhe. Jenista Muhagama akishirikishana jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango (katikati) na Waziri wa Nishati, Dkt. Merdard Kalemani wakati wa kikao cha majadiliano ya hoja za Mapendekezo ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2018/19, Hali ya Uchumi wa Taifa na Mpango wa Maendeleo wa Taifa leo Bungeni Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_33065" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akikabidhi Jozi ya Jezi kwa wachezaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya wanawake kutoka Jimbo la Kilolo leo Bungeni Jijini Dodoma. Wapili kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe na wapili kulia ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa, Mhe. Ritha Kabati.Timu hiyo ilitembelea Bunge kufuatia mwaliko wa Mbunge wao Venance Mwamoto (hayupo pichani).[/caption] [caption id="attachment_33066" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya wanawake kutoka Jimbo la Kilolo walipotembelea Bunge leo Jijini Dodoma. Kutoka kushoto kwa Waziri Mwakyembe ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa, Mhe. Ritha Kabati. Timu hiyo ilitembelea Bunge kufuatia mwaliko wa Mbunge wao Venance Mwamoto (wa kwanza kushoto).[/caption] [caption id="attachment_33067" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na wanakikundi cha wakulima wa zao la Parachichi kutoka mkoani Njombe walipofika Bungeni kwa mwaliko wa Mbunge wao Mhandisi. Geryson Lwenge (hayupo pichani) leo Jijini Dodoma. (Picha na: Frank Shija - MAELEZO, Dodoma)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi