Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mashine Mpya Kuongeza Uzalishaji Vitambulisho NIDA - Simbachawene
Apr 01, 2020
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_51949" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo katika Ukumbi wa wizara, jijini Dodoma ambapo ameahidi kuwashughulikia Watendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wasiotoa huduma stahiki kwa wananchi wanaofika kuomba vitambulisho[/caption]

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Serikali imenunua mashine mpya yenye thamani ya sh bilion 8.5 yenye uwezo wa kufyatua vitambulisho 9000 kwa saa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene alisema tayari Serikali imenunua mashine mpya ambazo zitakamilishwa kufungwa Aprili mwaka huu kwa ajili ya kuanza kufanya kazi.

Alisema mtambo huo mpya una uwezo wa kuzalisha vitambulisho 9, 000 kwa saa jambo ambalo kwa siku nzima wana uwezo wa kutoa vitambulisho vya kutosha kwa wananchi wake.

Alisema mitambo mipya na ikishirikiana na ile ya zamani wanaamini watatoa vitambulisho vingi ambapo wanatarajia kukamilisha zoezi hilo ndani ya miaka miwili.

"Safari hii vitambulisho vitakuwa bora, awali vilivyotolewa havikuwa na ubora kutokana na mashine kuwa chakavu, " alisema Simbachawene.

Alisema awali mtambo ulikuwa ukizalisha vitambulisho 500 lakini hivi sasa vitaboreshwa na kuzalishwa vitambulisho vingi kwa siku ili kukamilisha zoezi hilo.

Hata hivyo aliwaomba radhi wananchi kutokana na kupata shida katika zoezi hilo hivyo amewaahidi hivi sasa litafanyika kwa haraka zaidi.

Alisema mashine hizo ni bora na zitafanikiwa kukamilisha zoezi hilo ndani ya miaka miwili kwa watanzania wote au pungufu ya miaka hiyo.

Zoezi la utoaji vitambulisho linaendelea ambapo hadi sasa ni watu milioni sita pekee ndio wamekabidhiwa vitambulisho vya Taifa kati ya milioni 27. 7 waliotarajiwa kusajiliwa Mpaka sasa tayari NIDA imefanikiwa kutoa vitambulisho milioni sita na kutambua wananchi milioni 21. 8, hadi sasa kati ya watu 27.7 waliotarajiwa kusajiliwa.

Jumla ya namba za kipekee za utambulisho ni milioni 17. 8 zilikiwa zimezalishwa na zinaweza kutumika katika utambuzi wa watu.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi