Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (Mbele) akihutubia maelfu ya wanafunzi wa shule za Sekondari za jijini Arusha zinazoshiriki michuano ya Copa/UMISSETA, wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola hapa nchini, kwa ushirikiano na TAMISEMI, imefanya uzinduzi wa mashindano ya umoja wa Shule za Sekondari (Umisseta) kwa kanda ya Kaskazini, mkoani Arusha kwa kugawa vifaa vya michezo kwa shule mbalimbali za Sekondari za Serikali na binafsi.
Katika uzinduzi wa mashindano hayo jijini Arusha, kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid mwishoni mwa wiki, mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, ambapo aliishukuru kampuni ya Coca cola kwa udhamini kufanikisha michuano yam waka huu.
Kwa upande wake, Meneja Mauzo wa Coca-Cola Mkoa wa Arusha, Boniface Mwasi alisema kuwa kampuni hiyo imeona umuhimu wa kuibua vipaji vya michezo ndio maana wamejikita kufadhili michezo kama hiyo kwa vijana ikiwa ni katika kuisaidia Serikali katika azma yake ya kukuza michezo.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (Kushoto) akisalimia moja ya timu ya shule za sekondari kutoka mkoa wa Arusha, katika ufunguzi wa mashindano ya Copa Umisseta mkoani hapa yaliyofanyika mwisho wa wiki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, ambapo kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola iligawa vifaa mbali mbali vya michezo kwa shule za Serikali na binafsi kwa ajili ya ushiriki wa michuano ya mwaka huu.