Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mashindano ya John Stephen Akhwari International Marathon Kufanyika Kila Mwaka.
Jun 10, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_44041" align="aligncenter" width="986"] Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wanariadha pamoja na wananchi waliojitokeza katika Mashindano ya John Stephen Akhwari International Marathon yaliyofanyika Juni 09 Jijini Arusha yaliyokuwa na lengo la kumuenzi Mwanariadha John Stephen Akhwari ambaye ameletea heshima Taifa mwaka 1968 aliposhiriki mbio za Km 42 nchini Mexico. Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Riadha nchini ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Antony Mtaka na Kulia ni Mwanariadha huyo Mzee John Stephen Akhwari.[/caption]

Na Shamimu Nyaki -WHUSM

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameiagiza Idara ya Michezo ya Wizara hiyo kushirikiana na Waandaaji wa Mashindano ya John Stephen Akhwari International Marathon kufanya mashindano hayo kila mwaka ili kumuenzi Mwanariadha huyo aliyeliletea Taifa heshima kubwa.

Mhe. Mwakyembe ametoa agizo hilo jana Jijini Arusha wakati alipofungua mashindano hayo yaliyofanyika kwa lengo la kutambua na kuenzi mchango wa Mwanariadha huyo ambaye aliitangaza nchi kupitia mchezo huo mwaka 1968 huko nchini Mexico wakati aliposhiriki mbio za Km 42 ambapo licha ya kuumia goti wakati wa mbio alikataa kusitisha mbio hizo na kuendelea kukimbia hadi alipomaliza kitendo kilichoonekana kuwa ni cha kizalendo kwa nchi yake.

“Serikali inatambua mchango mkubwa uliofanywa na Mwanariadha huyu John Stephen Akhwari katika mchezo wa riadha ndio maana nimeiagiza Idara ya Michezo kuhakikisha kuwa mashindano haya yanafanyika kila mwaka ili kuenzi uzalendo wa Mzee Akhwari”, Alisema Dkt. Mwakyembe.

[caption id="attachment_44042" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akimkabidhi Mzee John Stephen Akhwari tuzo ya heshima kutokana na mchango wake mkubwa katika mchezo wa riadha hapa nchini mara baada ya kumalizika kwa Mashindano ya John Stephen Akhwari International Marathon yaliyofanyika Juni 09 Jijini Arusha yaliyokuwa na lengo la kumuenzi Mwanariadha huyo ambaye ameletea heshima Taifa mwaka 1968 aliposhiriki mbio za Km 42 nchini Mexico. Wanaoshuhudia ni viongozi wa Shirikisho la Riadha hapa nchini.[/caption]

Aidha Mhe. Mwakyembe amewataka wachezaji wote nchini kucheza na kushiriki mashindano mbalimbali kwa lengo la kufaidika katika maisha yao kwa kuwa michezo katika ulimwengu wa sasa ni ajira hivyo lazima waongeze juhudi zaidi ili waweze kujitangaza ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Riadha nchini Mhe. Antony Mtaka amesema kuwa Mkoa wa Simiyu ambao ndiye anaoungoza kama Mkuu wa Mkoa tayari umeanza kujenga shule maalum ya michezo ili kufundisha vijana wengi zaidi ambao watakuwa na uwezo pamoja na vipaji vizuri katika michezo.

Vile vile Mhe. Mtaka amesema kuwa mchezo wa Riadha umeendelea kufanya vizuri hapa nchini kutokana na vijana wengi kujitokeza kucheza mchezo huo na kuahidi kuwa Shirikisho la Riadha nchini lipo tayari kufundisha wanariadha ambao wapo tayari kujifunza.

[caption id="attachment_44043" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea cheti cha utambuzi wa mchango wake katika mchezo wa riadha kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Riadha nchini ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Antony Mtaka(kushoto) mara baada ya kumalizika kwa Mashindano ya John Stephen Akhwari International Marathon yaliyofanyika Juni 09 Jijini Arusha yaliyokuwa na lengo la kumuenzi Mwanariadha huyo ambaye ameletea heshima Taifa mwaka 1968 aliposhiriki mbio za Km 42 nchini Mexico. Kushoto ni Mzee John Stephen Akhwari.[/caption] [caption id="attachment_44044" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akimvalisha Medali mshindi wa kwanza wa mbio za Km 21 kwa wanaume Bw. Emmanuel Giniki katika mashindano ya John Stephen Akhwari International Marathon yaliyofanyika Juni 09 Jijini Arusha yaliyokuwa na lengo la kumuenzi Mwanariadha huyo ambaye ameliletea heshima Taifa mwaka 1968 aliposhiriki mbio za Km 42 nchini Mexico.[/caption]

Naye Mzee John Stephen Akhwari amewashukuru waandaaji wa mashindano hayo ambapo amesema kuwa yatasaidia kuongeza ushindani katika mchezo huo.

Mzee Akhwari ameendelea kusisitiza kuwa kila mchezaji anaposhiriki mashindano yoyote nje ya nchi ni lazima atambue kuwa anaiwakilisha nchi yake hivyo ni lazima apambane kwa nguvu zake zote.

Mzee John Stephen Akwari aliingia katika kumbukumbu za Mwanariadha bora na mwenye uzalendo baada ya kushiriki Mbio za Km 42 nchini Mexico ambapo akiwa katikati ya mbio aliumia goti na aliposhauriwa apumzike alikataa na kusema “Nchi yangu haikunituma maili 5,000 kuanza mbio, ilinituma maili 5,000 kumaliza mbio”.

Mashindano hayo  yameshirikisha mbio za Km 21, wanaume na wanawake, Mbio za Km 05 wanaume na wanawake pamoja na Km mbili na nusu kwa watoto ambapo washindi walipatiwa zawadi mbalimbali.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi