Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania Kuendelea Kupambana na Rushwa Mahakamani
Sep 25, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_15322" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CMJA) leo Jijini Dar es Salaam. Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Kujenga Mahakama shirikishi, inayowajibika na thabiti kiutendaji” (Picha na: Frank Shija)[/caption]

Na: Paschal Dotto

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa serikali inaendelea kuhakikisha Mahakama hazijihusishi na vitendo vya rushwa ili kutoa haki kwa mujibu wa Sheria.

Mh. Samia ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mkutano wa Chama cha majaji na mahakimu wa nchi za Jumuiya ya Madola uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania.

[caption id="attachment_15325" align="aligncenter" width="750"] Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akielezea jambo mbele ya washiriki wa mkutano wa wananchama wa Chama cha Majaji na Mahakimu kutoka nchi za Jumuiya ya Madola (CMJA) leo Jijini Dar es Salaam. Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Kujenga Mahakama shirikishi, inayowajibika na thabiti kiutendaji”[/caption] [caption id="attachment_15328" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania Mhe. Jaji Ignas Kitusi akifafanua jambo mbele ya washiriki wa mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CMJA) leo Jijini Dar es Salaam. Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Kujenga Mahakama shirikishi, inayowajibika na thabiti kiutendaji”[/caption]

‘Ninaamini, nia ya kujenga mahakama bora na yenye kuaminika kwa Tanzania haiwezi kutenganishwa na juhudi za serikali katika kuondoa umaskini na rushwa” amesisitiza Mh.Samia.

Aidha Makamu wa rais amesema kuwa kuna uhitaji mkubwa kwa nchi kuwa na mahakama huru, makini na yenye kuwajibika ipasavyo kwani mahakama huru ni msingi mzuri wa demokrasia.

Alisema kuwa pamoja na changamoto mbalimbali za mahakama uhuru wa mahakama  ambao ni umakini,uwajibikaji na utoaji haki kwa kufuata utawala wa sheria kwa wananchi wake uko palepale.

[caption id="attachment_15790" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CMJA) Jaji John Lounders wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa chama hicho leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma.  Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Kujenga Mahakama shirikishi, inayowajibika na thabiti kiutendaji”[/caption]

Kwa upande wa Tanzania Mhe. Samia amesema kuwa katika awamu ya tatu ya mapambano dhidi ya rushwa ambapo kwa awamu mbili zilizopita serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza malalamiko yaliyotokana na ukiukwaji wa haki.

Katika awamu ya tatu ya mkakati wa kupambana na rushwa utakaochukua miaka mitano kuanzia 2017 hadi 2022, Tanzania itachukua uzoefu kutoka kwenye mkuatno huu wa kimataifa kutoka kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya madola.

Kwa upande wake Jaji mkuu wa Tanzania Professa Ibrahim Juma alisema mahakama hiyo iko huru na inatekeleza majukumu yake pasipo  kuingiliwa na mtu yeyote na akaahidi kuendelea kubadilishana uzoefu na mahakama za nchi wanachama ili kuboresha utendaji kazi.

[caption id="attachment_15334" align="aligncenter" width="750"] Gavana wa Benki Kuu Tanzania Prof. Benno Ndulu (wa kwanza kushoto) na Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Othman Chande (wa pili) wpamoja na baadhi ya Majaji Wakuu kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya ya Madola akiwemo Jaji Mkuu wa Mahakama ya Juu ya Kenya Jaji Francis Maraga (aliyekaa juu) wakifuatilia mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CMJA) leo Jijini Dar es Salaam. Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Kujenga Mahakama shirikishi, inayowajibika na thabiti kiutendaji”[/caption]

Aidha Profesa Juma amesema Mahakama ya Tanzania kupitia majaji imekubaliana kuwa kila Jaji atatakiwa kuhukumu zaidi ya kesi 220 ambazo ni asilimia 38 ya kesi zilizoahirishwa mwaka 2012 hadi asilimia 5 Desemba 2016 na hii itafanyika kila mwaka ili kujipima wao wenyewe  kama moja ya malengo waliyojiwekea.

Akizungumzia mipango ya mahakama hiyo Profesa Juma amesema kuwa hadi kufikia mwaka 2020 mahakama hiyo itakuwa imekamilisha ujenzi wa  mahakama Kuu 13,mahakama za hakimu mkazi 14,mahakama za Wilaya 48,pamoja na mahakama za Mwanzo 100.

 Mkutano wa mwaka huu wa chama cha majaji na mahakimu wa nchi za jumuiya ya madola umefanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini tangu Tanzania ijiunge na chama hicho mwaka 1970.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi