Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mama Maria Nyerere Awaasa Vijana Kuthamini Michezo na Utamaduni
Oct 12, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_18946" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO ) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abassi akisikiliza jambo kutoka kwa Mama Maria Nyerere kuelekea kumbukizi ya miaka 18 ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa mahojiano maalum na Mjane huyo nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam leo.[/caption]

Na.Paschal Dotto

Mama Maria Nyerere amewaasa vijana kuzingatia utamaduni na michezo ili kuweka sawa akili yao na kuendelea na ujenzi wa taifa kwani michezo hukutanisha watu wengi na kuwawezesha kubadilishana mawazo yenye kujenga katika maisha.

Akizungumza leo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam, Mama Maria Nyerere alisema kuwa michezo ni hatua muhimu ya ukombozi wa fikra kwa vijana kwani wakizingatia michezo wataweza kufanya kazi na kujipatia mahitaji muhumi kama chakula na kuondokana na dhana ya utegemezi.

“Vijana wamajikita katika mambo maovu, sasa kitakachoweza kusaidia ni michezo kwani inawachangamsha, kuwakutanisha na kuweza kubadilishana mawazo mazuri na kwa sasa wanaendelea vyema na masuala haya ya michezo ambayo yanadumisha pia utamaduni,” alisema Mama Maria

Aidha, Mjane wa Hayati Baba wa Taifa alisema kuwa kwa sasa vijana wameanza kujirudi katika kudumisha utamaduni kwani walitaka kupotoka na kuacha utamaduni wao, alieleza kuwa watoto wanazaliwa bila ukomavu wa akili katika utamaduni, lakini pia hawapati elimu ya kutosha kutoka kwa wazazi kuhusu utamaduni matokeo yake ni kuishia kuwa na watu wenye tabia za ajabu.

“Kitakachoweza kuwasaidia vijana wetu ni kuwafundisha utamaduni wetu ili wawe na maadili kwani sasa hivi mtoto anazaliwa hapati elimu ya utamaduni wake, wazazi wametupa utamaduni mbali, ni lazima mtoto atakuwa na tabia za ajabu ajabu,”alisisitiza Mama Maria Nyerere.

Aliongeza  kuwa jukumu la ukombozi wa vijana kutoka katika vitendo vibovu ni la watanzania wote kuweza kuwaelimisha vijana kuhusu michezo ili kuweka akili zao sawa katika kuzalisha na kusaidia kujipatia  kipato chao na taifa kwa ujumla.

Mama Maria Nyerere alisema kuwa kujitegemea kwa vijana hasa katika kufanya kazi kutawawezesha kutimiza ndoto zao na za taifa lenye uchumi wa viwanda kwa ujumla.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi