Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makundi Maalum ya Vijana Shinyanga Yapatiwa Mafunzo ya Ujuzi Tepe
Jun 28, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) imetoa mafunzo ya ujuzi tepe ‘Soft Skills’ kwa makundi maalum ya vijana katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga yenye lengo la kujitambua na kujithamini.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo ya siku tatu yanayofanyika kuanzia leo Jumanne Juni 28,2022 hadi Juni 30,2022 katika ukumbi wa Liga Hotel Mjini Shinyanga, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bw. Julius Tweneshe amezitaja miongoni mwa mada zitakazofundishwa ni pamoja na kujitambua kama wajasiriamali, ujasiriamali na masoko.

Mada zingine ni urasimishaji wa biashara na usimamizi wa fedha, afya ya uzazi na ujinsia, afua zilizopo kwa ajili ya vijana wenye ulemavu na mama wadogo, afua zilizopo kwa ajili ya vijana wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.

“Vijana hawa pia watapewa mafunzo kuhusu fursa za uwezeshaji wa vijana kiuchumi ngazi ya taifa na mkoa, fursa za mitaji na huduma kwa wajasiriamali zinazotolewa Wataalamu kutoka taasisi mbalimbali, stadi za uongozi, taratibu za uundwaji wa vikundi,uundwaji wa vikundi vya uzalishajimali vya vijana, kubainisha mahitaji ya vikundi na uandaaji wa andiko mradi”,ameongeza Tweneshe.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi