Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Thobias Makoba, leo tarehe 28 Oktoba 2024, amefungua Kikao Kazi cha kuanzisha Kamati ya Kitaifa ya kumbukumbu za urithi wa dunia, kilichofanyika katika Hoteli ya Nashera jijini Dodoma.
Kamati hiyo inajumuisha wajunbe kutoka Idara ya Habari, UNESCO, Tume ya Taifa ya UNESCO, Wizara ya Maliasili na Utalii, Makumbusho ya Taifa, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, na Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar.