Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makatibu Wakuu Waridhishwa na Mradi wa Ghala la Mpunga Mvumi
Apr 22, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_52260" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe (aliyevaa kofia) alikagua mtambo wa kukoboa mpunga wa katika mradi wa ghala la kijiji cha Mvumi kilichopo wilayani Kilosa. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya.[/caption]

Na Mwandishi Wetu

Makatibu Wakuu wa Wizara nne leo wamefanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji mkoani Morogoro na kuridhishwa na kukamilika kwa ghala la kuhifadhia lililopo mpunga kijiji cha Mvumi Wilaya ya Kilosa.

Ziara hii imewashirikisha Makatibu Wakuu wa Wizara za Kilimo, Gerald Kusaya, Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe, Naibu Katibu Mkuu OR -TAMISEMI Bw. Gerlad Mweli na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais ,Mazingira,  Balozi Joseph Sokoine.

Akizungumza kwenye ukaguzi huo, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya alisema ghala la kijiji cha Mvumi limekamilika na muda si mrefu litakabidhiwa kwa wakulima ili litumike.

[caption id="attachment_52261" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya (aliemshika bega) akitoa maelekezo kwa mkandarasi mradi, Mhandisi Emanuel Norbet wa miundombinu ya Umwagiliaji Wilaya ya Kiliosa kukabidhi mradi ifikiapo 30 Aprili 2020. Mkataba wa kazi umemalizika tarehe 21 Aprili mwaka huu ambapo kazi imefikia asilimia 84.[/caption] "Wananchi wajipange kuanza kutumia ghala hili kwani kazi nzuri imefanywa na Serikali ya Awamu ya Tano kutoa fedha nyingi kujenga mradi huu ili usaidie kuongeza tija na thamani ya zao la mpunga kwa wakulima", alisema Bw. Kusaya. Mradi wa ujenzi wa ghala la kijiji cha Mvumi chini ya mradi wa Kuongeza Uwezo wa Uzalishaji wa zao la Mpunga (ERPP) hadi sasa umegharimu jumla ya shilingi Milioni 735 kati ya Milioni 971 zilizopangwa kukamilisha mradi huo ambao umefikia asilimia 99.3. Ghala Hilo lina uwezo wa kuhifadhi tani 1300 za mpunga kwa mwaka na litakuwa na kiwanda cha kukoboa mpunga chenye uwezo wa kukoboa kilo 1,200 kwa siku. [caption id="attachment_52262" align="aligncenter" width="750"] Ghala la kuhifadhia mpunga lililopo katika Kijiji cha Mvumi wilayani Kilosa lenye uwezo wa kuhifadhi tani 1300 kwa mwaka likiwa limekamilika kwa asilimia 99 kwa gharama ya shilingi milioni 735 kati ya milioni 971 chini ya mradi wa ERPP.[/caption]

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Gerlad Mweli amewataka wanakijiji wa Mvumi kujitolea kukamilisha ujenzi wa uzio wa ghala hilo ili kuimarisha ulinzi. ameshauri utaratibu uwekwe kwa kila mkulima atakayetunza mazao yake ghalani kuchangia fedha kidogo kwa ajili ya ujenzi wa uzio.

Naye mkulima James Nkalalwe wa kijiji hicho ameishukuru Serikali kwa kukamilisha mradi huo kwa sababu wanatarajia mradi huo utawaongezea tija na uchumi wa wakulima.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi