Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais Ataka Ushirikiano Zaidi Kisheria Kati ya Afrika na Asia
Oct 22, 2019
Na Msemaji Mkuu

Na. Paschal Dotto-MAELEZO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Samia Suluhu Hassan amezitaka nchi wanachama wa Shirika la Mashirikiano ya kisheria kwa nchi za Asia na Afrika (AALCO) kuimarisha ushirikiano na mshikamano katika kuendeleza sheria za kimataifa kwa manufaa ya nchi hizo.

Akizungumza katika Mkutano wa 58 wa Mwaka wa AALCO, uliofanyika Jijijni Dar es Salaam Makamu wa Rais amesema kuwa ni vizuri kwa taasisi hiyo ambayo inafanya kazi katika nchi za Asia na Afrika kuimarisha mshikamano ili kukuza sheria za kimataifa ambazo zitaleta Amani duniani.

“Napenda kuwaasa Nchi wanachama wa Shirika hili kuwa mnatakiwa kuendeleza Ushirikiano, Mshikamano na ushirikishwaji wa nchi zote katika masuala  ya kisheria ili kukuza na kuendeleza sheria za kimataifa kupitia Taasisi ya AALCO”, alisema Makamu wa Rais.

Aidha Makamu wa Rais alisema kuwa AALCO ina umuhimu mkubwa kwa nchi za Asia na Afrika kwani inaleta mapinduzi makubwa na kuendeleza sheria za kimataifa ambazo zinasaidia katika masuala mbalimbali ya kikanda.

[caption id="attachment_48230" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi akitoa utambulisho wa mkutano wa AALCO uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Aliyataja masuala hayo ni kama na kuimarisha Sheria za Biashara hususani kwenye biashara za kimataifa, kuleta umiliki wa mali kwa nchi husika na kulinda usalama wa kikanda katika nchi wanachama wa AALCO.

Mhe. Samia alisema kwamba mwaka 1956 ilikuwa na jukumu kubwa la kuendeleza ukuaji wa Sheria za kimataifa kwa bara za Asia na Afrika ambayo ilileta faida kubwa ya ukomavu wa Sheria katika ukanda huo.

“Mkutano huu ambao ni mara ya Kwanza kufanyika Tanzania unaonyesha jinsi gani Tanzania ilishiriki katika kukuza Sheria za kimataifa kwa Kushirikina na AALCO ambapo kupitia Shirika hilo Tanzania iliweza kusaidia kupatikana kwa uhuru kwa nchi za kusini mwa Afrika.

Pia alisemanchi yetu imekuwa nchi yenye Amani na majirani zake, imekuwa nchi ambayo inadumisha na kujenga Amani kwenye nchi mbalimbali, kwa hivyo ni dhahiri kuwa Tanzania inafanya kazi kwa karibu na AALCO kuendelea kufaidi matunda yake.

Kwa Niaba ya watanzania wote Mhe. Samia aliwakaribisha wageni waliofika katika mkutano kwani ni ishara ya kuendelea kumuunga mkono katibu Mtendaji wa AALCO Prof.Kennedy Gastorn tangu Aingie katika utendaji huo mwaka 2016.

[caption id="attachment_48231" align="aligncenter" width="750"] Washiriki wa Mkutano wa 58 wa Mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO).[/caption]

Aidha, Mhe. Samia alisema kuwa uzoefu wa Tanzania katika mikutano mbalimbali ya kisheria na ushuluhishi ikiwemo Mkutano wa Bandung na NAM umeiwezesha Tanzania kuwa msuluhishi na mjenzi mkuu wa Amani katika nchi mbalimbali, lakini pia Tanzania imekuwa ni nyumbani kwa wakimbizi wengi ambao nchi zao zina machafuko.

Alieleza kuwa katika hatua kubwa ya ushirikiano kati ya Tanzania na AALCO Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kupambana na rushwa, baishara haramu ya kusafirisha bidamu na utakatishaji fedha kwa nchi wanachama wa AALCO.

Makamu wa Rais aliwahakikishia wageni wa mkutano huo kuwa Tanzania ni nchi salama na yenye watu wenye ukarimu wa hali ya juu hivyo akawataka wasisite kuja kuitembelea kwani ina vivutio mbalimbali ambavyo havipatikani sehemu nyingine nyoyote duniani.

Pia aliwahakikishia  wajumbe kuwa nchi hii ni kituo kikubwa na kivutio kikubwa cha uwekezaji katika Nyanja mbalimbali za maendeleo, hivyo akawakaribisha kuja kuwekeza pamoja na kuja kufanya biashara.

[caption id="attachment_48229" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais Mhe. Samia_Suluhu_Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri kutoka nchi za Asia na Afrika wanachama wa AALCO katika ufunguzi wa Mkutano wa 58 wa Mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO).[/caption]

 

 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi