Makamu wa Rais Ashiriki Ufunguzi wa Mkutano wa Jumuiya ya Madola
Jun 24, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango leo tarehe 24 Juni, 2022 wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Patricia Scotland wakati alipowasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kigali kushiriki ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya za Madola (CHOGMU 2022) unaoendelea Kigali nchini Rwanda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 24 Juni, 2022 akishiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya za Madola (CHOGMU 2022) unaoendelea Kigali nchini Rwanda.