Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais Arejea Tanzania
Jan 12, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango tarehe 11 Januari 2022 akiwa nchini Malawi alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Organ Troika Summit) pamoja na Jamhuri ya Msumbiji na nchi zinazochangia vikosi katika jeshi la utayari la SADC lililopo nchini Msumbiji.

Akifungua mkutano huo, mwenyekiti wa Troika ambaye pia ni Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesisitiza umuhimu wa kuiunga mkono Jamhuri ya Msumbiji katika mapambano yake dhidi ya mashambulizi ya kigaidi yanayoendelea katika Jimbo la Cabo delgado Kaskazini mwa Msumbiji.

Amesema ni muhimu Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) kushirikiana katika kuimarisha ulinzi na usalama na kurejesha hali ya Amani na utulivu katika maeneo yalioathiriwa na mashambulizi ya ugaidi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi