Makamu wa Rais Arejea Nchini Tanzania Kutokea Nchini Rwanda
Sep 08, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Mhe. Vincent Biruta katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali wakati akirejea nchini Tanzania mara baada ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika uliofanyika nchini Rwanda. Tarehe 08 Septemba, 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma wakati akitokea Kigali Nchini Rwanda ambapo alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika uliofanyika nchini Rwanda. Tarehe 08 Septemba, 2022.