Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Mhe. Vincent Biruta wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali nchini Rwanda ambapo anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika wa Mwaka 2022 (AGRF 2022) unaofanyika nchini humo kuanzia tarehe 6 hadi 9 Septemba, 2022.