Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais Akishiriki Ibada leo Desemba, 2023
Dec 10, 2023
Makamu wa Rais Akishiriki Ibada leo Desemba, 2023
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na waumini mara baada ya kushiriki Ibada ya Jumapili katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege Dodoma leo tarehe 10 Desemba 2023.
Na Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma katika Ibada ya Jumapili leo tarehe 10 Desemba 2023. Ibada hiyo imeongozwa na Padre Dionis Paskal Safari.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki Ibada ya Jumapili katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege Dodoma leo tarehe 10 Desemba 2023.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo, Makamu wa Rais amewaasa Watanzania kutumia vema mitandao ya kijamii. Amesema matumizi yasiyofaa ya mitandao ya kijamii yamekuwa yakiumiza watu wengi hivyo yampasa kila mmoja kutumia vema pamoja na kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Mapadre mara baada ya kushiriki Ibada ya Jumapili katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege Dodoma leo tarehe 10 Desemba 2023.

Makamu wa Rais amewashukuru waumini hao kwa kuendelea kumuombea ili aweze kutekeleza vema majukumu yake.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na kaka yake, Padre Sebastian Mpango (kushoto) pamoja na Padre Emmanuel Mtambo (kulia) mara baada ya kushiriki Ibada ya Jumapili katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege Dodoma leo tarehe 10 Desemba 2023.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi