Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais Akagua Daraja la Nyeburu
Jun 17, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amewaasa wakandarasi wazawa kutumia vema na kwa ufanisi fursa wanazopewa na serikali za ujenzi wa mirad imbalimbali ili kuendelea kupewa nafasi hizo zaidi.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati aliposimama na kukagua ujenzi wa daraja la Nyeburu linalounganisha eneo la Pugu na Chanika Jijini Dar es Salaam ambalo ujenzi wake umekuwa ukisuasua. Makamu wa Rais ameonesha kutofurahishwa na maendeleo ya ujenzi huo ambapo amaesema ujenzi wa daraja hilo umechukua muda mrefu na kuathiri wananchi hasa wakati wa mvua licha ya serikali kuendelea kutoa malipo kwa wakati kwa mkandarasi katika kila kazi.


Aidha, Makamu wa Rais amesema serikali imeendelea kuwapa kipaumbele wakandarasi wa ndani kutokana na kutambua wanafahamu vema changamoto zinazosababishwa na ubovu wa miundombinu hivyo wanapaswa kutekeleza majukumu yao kiufanisi zaidi.

Pia Makamu wa Rais amewataka  Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) pamoja na TANROADS kuwasimamia kikamilifu wakandarasi ili wakamilishe miradi kwa wakati na kuokoa fedha za walipa kodi wa Tanzania.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi