Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais Akabidhi Zawadi kwa Watoto Yatima
Dec 23, 2023
Makamu wa Rais Akabidhi Zawadi kwa Watoto Yatima
Msaidizi wa Sheria wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Elisha Suku (mwenye koti jeusi) akikabidhi zawadi kutoka kwa Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Mpango katika Kituo cha kulea Watoto Yatima cha Jerusalem Home of God’s Love For Children kilichopo Kimara Jijini Dar es salaam. Watatu kutoka kushoto ni Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Kimara Jijini Dar es salaam, Wilbroad Matsai. Tarehe 23 Desemba, 2023.
Na Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango amekabidhi zawadi katika Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Jerusalem Home of God’s Love For Children kilichopo Kimara jijini Dar es salaam. Zawadi hizo ni pamoja na vyakula, vinywaji, sabuni, mafuta ya kupikia pamoja na mavazi. 

 

Akikabidhi zawadi hizo Msaidizi wa Sheria wa Makamu wa Rais, Bw. Elisha Suku amesema Makamu wa Rais ametoa zawadi hizo kwa lengo la kusheherekea pamoja na watoto hao sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya. Aidha ameongeza kwamba Makamu wa Rais amewatakia heri na afya njema watoto pamoja na walezi wao.

Akizungumza mara baada ya kupokea zawadi hizo, Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Kimara jijini Dar es salaam, Wilbroad Matsai amemshukuru Makamu wa Rais kwa zawadi hizo pamoja na viongozi wote wanaojitoa kwa ajili ya kusaidia wenye uhitaji.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi