Majaliwa Azindua Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISETA Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora
Aug 04, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Fazal Mohammed kutoka Tanga ambaye ni mchezaji wa mpira wa wavu wakati alipozindua Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISETA kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora, Agosti 4, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na viongozi wakishuhudia maandamano ya washiriki wa Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) wakati alipozindua mashindano hayo kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora, Agosti 4, 2022. Kulia ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul, wa tatu kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, David Silinde na wa nne kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi, Dkt. Batilda Burian
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas nakala za vitabu vya miongozo na mikakati kwa ajili ya kuboresha elimu nchini inayolenga kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazoathiri sekta ya elimu. Makabidhiano hayo yalifanyika wakati Waziri Mkuu alipozindua Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari Tanzania ( UMISETA kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora, Agosti 4, 2022. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, David Silinde
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua timu ya mpira wa pete ya Mkoa wa Kagera wakati alipozindua Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISETA kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora, Agosti 4, 2022.
Wanamichezo kutoka Pemba wakiandamana mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozindua Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISETA kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora, Agosti 4, 2022.
Wanamichezo kutoka Mkoa wa Morogoro wakiandamana mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozindua Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISETA kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora, Agosti 4, 2022.