Majaliwa Azindua Jengo la Huduma ya Macho Katika Hospitali Ya Rufaa Ya Kanda Bugando Jijini Mwanza
Oct 16, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Askofu wa Jimbo la Geita , Flavian Kasalaa (wa tatu kushoto) wakizindua jengo la Huduma ya Macho katika Hospital ya Rufaa ya Kanda Bugando jijini Mwanza Oktoba 16, 2022. Wa pili kulia ni Askofu Mkuu, Renatus Nkwande wa Jimbo Kuu la Mwanza, kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula, wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua jengo la Huduma ya Macho katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando jijini Mwanza, Oktoba 16, 2022. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula, Mkurugenzi wa Wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Dkt. Fabian Massaga, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Askofu wa Jimbo la Geita, Flavian Kassala, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Renatus Nkwande, Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Christian Blind Mission ya Ujerumani, Nesia Mahenge na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Dkt. Christopher Mwanansao ambaye ni Mkuu wa Idara ya Macho katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando wakati alipozindua jengo la Huduma ya Macho katika hospitali hiyo jijini Mwanza, Oktoba 16, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja watumishi wa Taasisi ya Christian Blind Mission ya Ujerumani baada ya kuzindua jengo la Huduma ya Macho katika hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando jijini Mwanza, Oktoba 16, 2022. Kushoto kwake ni Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katolika Tanzania (TEC) na Askofu wa Jimbo la Geita, Flavian Kassala na kulia kwake ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Renatus Nkwande.