Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary Majaliwa (kulia) wakisalimiana na viongozi wa Mkoa wa Ruvuma wakati walipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Songea kwa ziara, Januari 2, 2022. Kutoka kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Songea Mjini, Dkt. Damas Ndumbaro, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo, Oddo Mwisho na wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Ruvuma baada ya kupokea Taarifa ya Maendeleo ya Mkoa huo kwenye uwanja wa ndege wa Songea, Januari 2, 2022. Wa pili kushoto ni Mkewe Mary Majaliwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary Majaliwa (kulia) wakiagana na viongozi wa Wilaya ya Ruangwa kabla ya kuondoka wilayani humo kuelekea Songea kwa ziara Mkoani Ruvuma, Januari 2, 2022.