Majaliwa Amwakilisha Rais Samia Katika Mazishi ya Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe
Sep 27, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wa pili kushoto) wakiweka maua wakati wa mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa Waziri Mkuu Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe yaliyofanyika Tokyo nchini Japan Septemba 27, 2022. Kushoto ni mke wa Balozi wa Tanzania nchini Japan, Consolata Luvanda na kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa mkono wa pole mjane wa Waziri Mkuu mstaafu, Shinzo Abe, Bibi Akie Abe, kwenye Kasri la Kifalme la Akasaka, jijini Tokyo Japan, Septemba 27.2022. Baada ya kutoa heshima za mwisho kwa Waziri Mkuu mstaafu wa nchi hiyo, Bw. Shinzo Abe
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ameongozana na mkewe Mery Majaliwa wakimpa mkono wa pole Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida kwenye Kasri la Kifalme la Akasaka, jijini Tokyo Japan, Septemba 27.2022. Baada ya kutoa heshima za mwisho kwa Waziri Mkuu mstaafu wa nchi hiyo, Bw. Shinzo Abe.