Majaliwa Akagua Madarasa Yaliyojengwa na Serikali Katika Shule ya Sekondari Irugwa
Oct 17, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi leo Oktoba 17, 2022 baada ya kukagua madarasa sita katika Shule ya Sekondari Iirugwa wilayani Ukerewe yaliyojengwa kwa Shilingi milioni 120 zilizotolewa na Serikali Kuu ambazo zilibaki na zikatumika kujenga matundu ya vyoo, mabafu na mfumo wa kuvuna maji ya mvua na umeme wa sola, Pia zilitumika kununua madawati.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama madawati wakati alipokagua madarasa sita katika Shule ya Sekondari Irugwa wilayani Ukerewe ambayo yamejengwa kwa Shilingi milioni 120 zilizotolewa na Serikali Kuu ambazo zilibaki na zikatumika kujenga matundu ya vyoo, mabafu na mfumo wa kuvuna maji ya mvua na umeme wa sola, Oktoba 17, 2022. Pia zilitumika kununua madawati.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watoto Katondo Kebele (kushoto), Wilhelemina Mafele (katikati ) na Gozibert Bwere ambao walishiriki kucheza ngoma ya kikundi cha Utandawazi cha Ukerewe katika mkutano wa hadhara aliouhutubia katika uwanja wa michezo wa Shule ya Sekondari Irugwa wilayani Ukerewe Oktoba 17, 2022.