Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) kuongeza ufanisi katika Mipango na Bajeti.
Jun 08, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na Daudi Manongi,Iringa

Maafisa Ugavi kutoka  Halmashauri na Manispaa  Mikoa ya Iringa,Morogoro,Tanga na Kilimajaro wameaswa kuongeza ufanisi  kwa kutumia  Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) katika maeneo yao ya kazi.

Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa mafunzo hayo Meneja wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Mkoa wa Iringa Bw.Baraka Mwambene amewataka washiriki wa mafunzo hayo kutumia mfumo huu katika kufanya mipango na bajeti  katika maeneo yao.

Meneja wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Mkoa wa Iringa Bw.Baraka Mwambene akifungua mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) kwa Maafisa Ugavi  wa Halmashauri na Manispaa kutoka Mikoa ya Iringa,Morogoro,Tanga na Kilimajaro yaliyoanza leo Mkoani Iringa.

“Mamlaka zote za Serikali za Mitaa nchini Tanzania zitatumia mfumo mmoja wa uhasibu ujulikanao kama Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma, tolea la 10.2 (Epicor10.2), utakaosaidia kuhakikisha kuna mfanano katika uhasibu, utoaji taarifa na usimamizi wa fedha”.Aliongeza Bw.Mwambene.

Aidha amesema  mafunzo haya ni nafasi ya pekee katika  kubadilishana taarifa na Mfumo wa Mipango na Bajeti wa PlanRep na ule wa uhasibu na kutoa taarifa za fedha za vituo vya kutoa huduma, FFARS

Aidha kwa upande wake Mhasibu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw.Juma Shaha ameeleza faida kubwa za kutumia mfumo huo  kuwa  utaongeza uwazi katika kupanga mipango na bajeti.

Meneja wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Mkoa wa Iringa Bw.Baraka Mwambene akijadili jambo na mshiriki wa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) kwa Maafisa ugavi  yaliyoanza leo Mkoani Iringa.

Pili mfumo huu utaongeza ushirikiano kwani mfumo huu utashushwa hadi kwenye ngazi ya mtoa huduma na pia  matumizi yote yanayofanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa vituo vyake vya afya na shule yatahifadhiwa na kuwekwa wazi kwa vituo vya kutolea huduma pamoja na jamii wanayoitumikia.

Aidha mfumo huu utaondoa changamoto za utoaji wa taarifa hasa kutoka kwenye vituo vya kutolea huduma pamoja na kuunganisha taarifa hizo kwenye Hesabu za Halmashauri, pia utatoa taarifa za utekelezaji za mipango na bajeti kwa kuzingatia matumizi ya fedha yaliyofanyika.

Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), ni Mradi wa miaka mitano unaotekelezwa katika mikoa 13 na Halmashauri 93 za Tanzania bara.  PS3 inafanya kazi katika sekta mbalimbali ili kuimarisha mifumo ya mawasiliano, utawala bora, fedha na rasilimali watu, hususani kwa jamii zenye uhitaji.

Baadhi ya Washirika wa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo hayo yanayoshirikisha Maafisa ugavi kutoka Mikoa ya Iringa,Morogoro,Tanga na Kilimajaro yaliyoanza leo Mkoani Iringa.

Baadhi ya Washirika wa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo hayo yanayoshirikisha Maafisa ugavi  kutoka Mikoa ya Iringa,Morogoro,Tanga na Kilimajaro yaliyoanza leo Mkoani Iringa.

Mhasibu kutoka Mkoa wa Songwe Bw.David Johnson akielezea  umuhimu wa  Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma wakati wa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) kwa Maafisa ugavi kutoka Mikoa ya Iringa,Morogoro,Tanga na Kilimajaro yaliyoanza leo Mkoani Iringa.

Mhasibu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI  Bw.Juma Shaha akitoa maelezo jinsi mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) unavyofaya kazi wakati wa mafunzo ya mfumo huo kwa maafisa ugavi leo Mkoani Iringa.

Afisa Ugavi kutoka Wilaya ya Muheza Bi.Furaha Sarakikya akifanya mazoezi kwa vitendo jinsi ya kutumia mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) wakati wa mafunzo ya mfumo huo yaliyoanza leo Mkoani Iringa

Mhasibu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI  Bw.Juma Shaha akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo ya mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) yanayofanyika mkoani Iringa yakijumuisha Maafisa ugavi  kutoka Mikoa ya Iringa,Morogoro,Tanga na Kilimajaro.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi