[caption id="attachment_36545" align="aligncenter" width="764"] Sehemu ya Washiriki wakiwa katika mafunzo ya Mahakimu na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata mkoani Tabora.[/caption]
Na Aisha Abdallah, Mahakama Kuu Tabora
Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Mhe. Salvatory Bongole amefungua rasmi Mafunzo ya Mahakimu na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata mkoani humo yanayolenga kuwajengea uwezo wa kuyasimamia mabaraza ya kata katika utekelezaji wa majukumu kwa mujibu wa sheria.
Akifungua Mafunzo hayo mapema Oktoba 08, katika Ukumbi wa Katibu Tawala, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. Bongole aliwaelezea washiriki wa mafunzo hayo kuwa ni muhimu kwa sababu yataleta uelewa wa pamoja kati ya Mahakama na Mabaraza ya Kata juu ya mamlaka ya Mahakama na Mabaraza katika utoaji haki.
Aidha katika hotuba yake ya ufunguzi, Mhe. Jaji Mfawidhi huyo pia alisisitiza kuhusu umuhimu wa kumsikiliza mtu kabla ya kutoa maamuzi na kuwaasa wanasemina kuyatekeleza mambo yote watakayojifunza katika semina hiyo.
[caption id="attachment_36544" align="aligncenter" width="750"]