Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mabenki Yaaswa Kukopesha Sekta ya Kilimo
Jun 19, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_3838" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Augustino Chacha akizungumza wakati akifungua mafunzo ya awamu ya pili yanayohusiana na Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo. Mafunzo hayo ya awamu ya pili yatafanyika kwa siku sita yanaendeshwa kwa pamoja kati ya TADB, NABAD na MIVARF.[/caption]

Na Saidi Mkabakuli- RS TADB.

Mabenki yameombwa kuwa tayari kukopesha mnyororo mzima wa sekta ya kilimo na mifugo ili kuunga mkono juhudi  za Serikali za kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Augustino Chacha wakati akifungua mafunzo ya awamu ya pili yanayohusiana na kanuni za ukopeshaji katika Kilimo yanayoendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya TADB, Benki ya Taifa ya Kilimo na Maendeleo Vijijini India (NABAD),  Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani Mazao na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).

Chacha amesema kuwa mabenki na taasisi za kifedha nchini hazina budi kuwekeza ili kuwa na mtaji wa kutosha kuweza kukopesha sekta ya kilimo ambayo ni uti wa mgongo wa Tanzania, inayoajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya  asilimia 65 cha malighafi kwa ajili ya viwanda vilivyoko nchini.

[caption id="attachment_3847" align="aligncenter" width="750"] Meneja Msaidizi wa Mafunzo kutoka NABAD, Dkt. R.S. Reddy akifundisha namna ya kufanyia uchambuzi miradi ya kilimo ili kuongeza tija kwenye utoaji wa mikopo kwenye sekta hiyo.[/caption] [caption id="attachment_3841" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Idara ya Majanga na Vihatarishi, Bw. Adam Kamanda (kulia) akizungumza nafasi ya TADB katika kuwezesha Mabenki na Taasisi za Fedha nchini kuweza kukopesha wakulima.[/caption] [caption id="attachment_3844" align="aligncenter" width="750"] Washiriki wa Mafunzo ya Awamu ya Pili ya Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo wakiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi na viongozi kutoka TADB.[/caption]

Ameongeza kuwa kuanzishwa kwa TADB kunalenga kuwezesha mabenki ya biashara kupata fedha zenye masharti nafuu na endelevu ili ziweze kukopesha sekta ya kilimo ili kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

“Hakuna haja ya kuogopa kukopesha sekta ya kilimo kwani ni sekta yenye umuhimu mkubwa kwenye uchumi wa nchi yetu, TADB kama benki kiongozi  ya maendeleo ya kilimo, pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi nyingine za kifedha kutoa fedha kwenye mnyororo mzima wa kilimo, imejipanga kusaidia upatikanaji wa fedha zenye masharti nafuu na endelevu, ili kuinua ushiriki wa wakulima wadogo katika mfumo wa kifedha,” alisema Chacha.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Majanga na Vihatarishi, Adam Kamanda kwa kutambua umuhimu wa kuendeleza sekta ya kilimo TADB imejipanga kuwa benki ya mfano na ya kisasa katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania, kutoka kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo cha kibiashara na uzalishaji wenye tija katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

Kamanda ameongeza kuwa TADB imejipanga kupunguza changamoto za ukopeshaji zinazoikabili sekta ya kilimo nchini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi