Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Maafisa Lishe Waaswa Kuelimisha Wananchi Umuhimu wa Chakula Bora
Oct 05, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_47632" align="aligncenter" width="750"] Katibu mkuu , Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi Dorothy Mwaluko akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mkutano wa wadau wa lishe Jijini Dodoma Oktoba 4,2019 kwa niaba ya Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri mkuu, Kazi Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mhe. Jenista Mhagama.[/caption]

Na Mwandishi wetu- Dodoma

Maafisa lishe nchini wametakiwa kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuzingatia lishe bora ili kuondoa changamoto ya utapiamlo na udumavu  katika  jamii.

Akizungumza wakati akifunga mkutano wa siku mbili wa wadau wa lishe uliofanyika Jijini Dodoma  Oktoba  4, 2019 kwa niaba ya Waziri wa  nchi, Ofisi  Waziri mkuu, Kazi Vijana Ajira  na Wenye Ulemavu mhe.  Jenista Mhagama, Katibu mkuu Ofisi ya Waziri mkuu  anayeshughulikia  Sera Uratibu na Uwekezaji Bi. Dorothy Mwaluko amesema kuwa maafisa lishe wanapaswa kuongeza juhudi katika kutoa elimu kwa kushirikiana na wadau kuhusu  umuhimu wa lishe bora.

“ Kipaumbele lazima kiwekwe katika makundi maalum kama wazee,  watoto,  akinamama wanajawazito na wale wanaonyonyesha ili kufanikisha azma ya Serikali kuondoa Changamoto ya utapiamlo na udumavu hapa nchini”; Alisisitiza Bi. Mwaluko.

Akifafanua amesema kuwa Serikali inasisitiza matumizi ya sanaa, vyombo vya habari na viongozi wa kisiasa wakiwemo wabunge katika kuelimisha umma kuhusu  athari za utapimlo na udumavu hapa nchini.

[caption id="attachment_47633" align="aligncenter" width="750"] Katibu mkuu , Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya) Dkt. Zainab Chaula akieleza umuhimu wa lishe bora na hatua zitakazochukuliwa na Wizara hiyo ili kuhakikisha kuwa suala hilo linapewa kipaumbele kuwezesha changamoto ya utapiamlo na udumavu kupatiwa ufumbuzi kwa ushirikiano na wadau.[/caption]

Kwa upande wake Katibu mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto (Afya) Dkt. Zainab  Chaula amesema kuwa  maazimio ya kikao hicho yanapaswa kutoa majawabu yatakayowezesha kuondokana na utapiamlo na udumavu hapa nchini.

Aliongeza kuwa Serikali imeweka mazingira wezeshi ya kufanya kazi na wadau katika kukabiliana na changamoto ya utapiamlo na udumavu katika maeneo yote nchini ili kujenga jamii yenye afya bora.

Aidha, Dkt. Chaula aliwataka washiriki wa mkutano huo kuhakikisha kuwa kila mmoja anakuwa sehemu ya mapambano dhidi ya utapiamlo na udumavu hapa nchini ili kujenga jamii yenye afya bora hasa wakati huu Taifa linapojenga   uchumi wa Viwanda na kutekeleza azma ya kuleta ustawi kwa wananchi.

Kikao kazi cha wadau wa lishe kimefanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma  kikiwashirikisha wadau wa maendeleo, Maafisa lishe, Viongozi wa Serikali wakiwemo Mawaziri, Makatibu wakuu, Wabunge na Taasisi mbalimbali za Serikali  na zisizo za kiserikali.

[caption id="attachment_47634" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Germana Leyna akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kufunga mkutano wa wadau wa lishe Oktoba 4, 2019 Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_47635" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya washiriki wa mkutano wa wadau wa lishe wakifuatilia hafla ya kufungwa kwa mkutano huo Oktoba 4, Jijini Dodoma, mkutano huo ulifungwa na Katibu mkuu , Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi Dorothy Mwaluko kwa niaba ya Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama.[/caption]

(Picha zote na Frank Mvungi)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi