Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Maafisa JWTZ Watembelea Ubalozi wa Tanzania Nchini Italia
Feb 04, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiongozwa na Mkuu wa Kurugenzi ya Intelijensia Makao Makuu ya Jeshi, Maj. Gen. Ramadhani Mrangira pamoja na Col. Abdallah Khalfan wametembelea Ubalozi wa Tanzania Jijini Roma, Italia.

Wakiwa Ubalozini walipokelewa na mwenyeji wao Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ambapo pamoja na mambo mengine wamezungumzia masuala ya ushirikiano. Maafisa hao walikuwepo nchini Italia kwa shughuli za kikazi. 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi