Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Maafisa Habari Watakiwa Kutumia Vyema Taaluma Zao
Oct 06, 2023
Maafisa Habari Watakiwa Kutumia Vyema Taaluma Zao
Katibu Mkuu wa Chama cha Maafisa Habari wa Serikali (TAGCO), Bw. Abdul Njaidi akizungumza leo Oktoba 6, 2023 wakati wa uhitimishaji wa Mafunzo ya kuboresha mawasiliano ya Kidijitali ya siku tano yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) kwa kushirikiana na TAGCO, jijini Mwanza,
Na Mwandishi wetu

Katibu Mkuu wa Chama cha Maafisa Habari wa Serikali (TAGCO), Bw. Abdul Njaidi amewataka Maafisa Habari Serikalini kufanya kazi kwa ufanisi na weledi, ili kuimarisha utoaji taarifa za Serikali kwa umma.


Akizungumza Oktoba 6, 2023 wakati wa uhitimishaji wa Mafunzo ya kuboresha mawasiliano ya Kidijitali ya siku tano yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) kwa kushirikiana na TAGCO, jijini Mwanza, Njaidi amesema Maafisa Habari wana jukumu kubwa katika kutangaza utekelezaji wa shughuli za Serikali kupitia taasisi zao.


“Msipotangaza, wananchi wanabaki bila kuelewa nini kinafanyika. Matokeo yake ni malalamiko na lawama kwa Serikali,” amesema.


Aidha, Bw. Njaidi amesisitiza utoaji wa taarifa za mara kwa mara, uhuishaji wa tovuti na mitandao ya kijamii na kushirikiana kwa karibu na vyombo vya habari ili kupanua wigo wa usambazaji wa habari kwa umma.


Sambamba na hilo, Bw. Njaidi amewataka maafisa hao kujenga mshikamano miongoni mwao na kushirikiana katika utendaji kazi ili kuongeza ufanisi. 


Mafunzo ya KidiJitali kwa Maafisa Habari yalihusisha mada mbalimbali zikiwemo za Uandaaji na Uhariri wa Habari Kidijitali, Stadi za Uongozi na Usimamizi wa Vitengo vya Mawasiliano, Uandaaji na Uwasilishaji wa Hotuba, na Matumizi bora ya Mitandao ya Kijamii.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi