Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini watakiwa kujenga timu ya ushirikiano
May 24, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_32147" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Mkoani Arusha Christopher Kazeri (katikati) akizungumza na Uongozi wa Chama cha Maafisa Habari Serikalini (TAGCO) na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi wakati wa ziara yao ya kutembelea Kitengo vya Habari na Mawasiliano Serikali katika Halmashauri hiyo jana Jumatano Mei 23, 2018.

[/caption] [caption id="attachment_32148" align="aligncenter" width="750"] Katibu wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Abdul Njaidi katikati akichangia hoja wakati wa mkutano baina ya TAGCO na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru iliyolenga kujionea utendaji kazi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Halmnashauri hiyo jana Jumatano Mei 23, 2018.[/caption]

Na Mwandishi Wetu, MAELEZO, ARUSHA

MAAFISA Habari na Mawasiliano Serikalini  wametakiwa kujenga timu ya ushirikiano wa pamoja na Wataalamu wa kada mbalimbali waliopo katika maeneo yao ya kazi ili kutangaza vyema mafanikio ya miradi na program zilizotekelezwa na zinazotekelezwa na Serikali.

Hayo yamesemwa jana Mkoani Arusha na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati wa mwendelezo wa ziara yake ya siku tano ya kutembelea na kujionea utendaji kazi wa Vitengo vya Habari na Mawasiliano Serikalini katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali za Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Dkt. Abbasi alisema malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa watendaji wote wa Serikali wanakuwa mstari wa mbele katika kuwaletea maendeleo ya haraka  wananchi wake kwani Serikali inajenga nyumba moja, hivyo ni wajibu wa watumishi wote kuungana pamoja katika kusukuma mbele gurudumu hilo hususani katika maeneo ya Mikoa na Halmashauri ambapo Serikali hupeleka kiasi kikubwa cha pesa za miradi ya maendeleo.

[caption id="attachment_32149" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akichangia hoja wakati wakati wa mkutano baina ya TAGCO, Idara ya Habari (MAELEZO) na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru iliyolenga kujionea utendaji kazi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Halmnashauri hiyo jana Jumatano Mei 23, 2018.
[/caption] [caption id="attachment_32150" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Christopher Kazeri akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi na Mjumbe wa TAGCO, Innocent Byarugaba mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao uliolenga kujionea utendaji kazi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Halmnashauri hiyo jana Jumatano Mei 23, 2018.
[/caption] [caption id="attachment_32151" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Christopher Kazeri (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa TAGCO wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Paschal Shelutete mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina yao uliofanyika jana Mei 23, 2018 kwa ajili ya kujionea utendaji kazi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Halmashauri hiyo.[/caption]

“Katika Serikali ya Awamu ya Tano, ukiwa Afisa Mifugo, Nyuki, Maliasili, Tehama na wengineo tunawajibika kushirikiana kwa karibu zaidi na Maafisa Habari na Mawasiliano kwa kuwa shughuli zao zinahusu maendeleo ya wananchi, hivyo ni wajibu wa taarifa zao ziwafikie wananchi kwa wakati ili kuweza kujibu hoja na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali” alisema Dkt. Abbasi.

Aidha Dkt. Abbasi alisema Serikali tayari imetoa maelekezo kwa Watendaji Wakuu wa Mikoa na Halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa Maafisa Habari na Mawasiliano wanashirikishwa kwa karibu zaidi katika kupata taarifa mbalimbali za maeneo yao ya kazi ikiwemo kushiriki katika vikao vya juu vya maamuzi katika Mikoa, Halmashauri, Wizara, Taaasisi na Wakala.

Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema Maafisa Habari Habari na Mawasiliano katika Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kutengeneza majukwaa mbalimbali ya utoaji wa taarifa zao kwa umma ikiwemo matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kujibu hoja za kwa wanaopinga maendeleo yanayofikiwa na Serikali kwa wananchi wake.

[caption id="attachment_32152" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Christopher Kazeri (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi na Uongozi wa Chama cha Maafisa Serikali (TAGCO), mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina yao jana Mei 23, 2018 uliolenga kujoinea utendaji kazi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalimni katika Halmashauri hiyo.
[/caption] [caption id="attachment_32153" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi akiongoza kikao cha pamoja na Watendaji wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Maafisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Mkoani Arusha wakati wa ziara ya pamoja iliyoratibiwa na TAGCO Kwa ajili ya kujonea utendaji kazi wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika Halmashauri hiyo jana Jumatano Mei 23, 2018.[/caption]

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Mkoani Arusha, Christopher Kazeri alisema Halmashauri hiyo imefanya jitihada mbalimbali za kujenga ushirikiano baina ya Wakuu wa Idara za Halmashauri hiyo na Kitengo cha Habari na Mawasiliano hususani katika kuratibu shughuli za utoaji wa taarifa mbalimbali za matukio katika Halmashauri hiyo.

“Kwa sasa Afisa Habari wetu anashiriki katika kikao chetu cha juu cha kila mwezi katika Halmashauri ambacho kinaelezea utekelezaji wa miradi, kazi na majukumu mbalimbali, ambapo kwa kufanya hivyo tumeweza kufanya vizuri katika uwekaji wa taarifa sahihi na za wakati katika tovuti yetu ya Halmashauri” alisema Kazeri.

Aidha Kazeri alisema Ofisi yake pia imepanga kuweka mipango na mikakati mbalimbali ya kuimarisha kitengo cha Habari na Mawasiliano katika Halmashauri hiyo kwa kuhakikisha kuwa watendaji wake wanapata mafunzo ya mara kwa mara ili kuweza kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao.

[caption id="attachment_32154" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro Yohana Sintoo (katikati) akizungumza na Watendaji wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikali pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi (wa kwanza kushoto) wakati walipofika Ofisini kwake kujionea utendaji kazi wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika Halmashauri hiyo jana Jumatano Mei 23, 2018.
[/caption] [caption id="attachment_32155" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro Yohana Sintoo mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao hapo jana Mei 23, 2018 baina ya TAGCO kwa pamoja na Idara ya Habari (MAELEZO) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi (katikati).
[/caption] [caption id="attachment_32156" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Paschal Shelutete akizungumza katika mahojiano ya kipindi maalum cha Redio Boma FM ya Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara ya TAGCO na Idara ya Habari (MAELEZO) kujiounea utendaji kazi wa Kitendo cha Habari na Mawasiliano katika Halmashauri hiyo jana Mei 23, 2018. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt Hassan Abbasi.[/caption]

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Paschal Shelutete malengo ya ziara hiyo ni kujionea changamoto mbalimbali zinazowakabili Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali na hivyo kuweza kuwa na mikakati iliyo bora zaidi katika kuisemea na kutangaza mafanikio ya Serikali katika maeneo yao ya kazi.

Aliongeza kuwa TAGCO kwa kushiriana na Idara ya Habari (MAELEZO) imekusudia kufanya ziara hiyo kwa Maafisa Habari na Mawasiliano wote nchini ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na uelewa wa pamoja katika kuwa na njia na namna bora zaidi ya kubuni mikakati ya kuisemea Serikali.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi