Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Lowassa Alikuwa Mlezi wa Vijana
Feb 14, 2024
Lowassa Alikuwa Mlezi wa Vijana
Vijana waendesha pikipiki wakitoa heshima wakati mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowassa ukipititishwa katika baadhi ya maeneo mkoani Arusha ili wananchi waweze kumuaga
Na Lilian Lundo - MAELEZO

Vijana wa Wilaya ya Monduli wamesema Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowassa alikuwa mlezi wa vijana wa wilaya hiyo, ambapo alikuwa akiwaelekeza namna ya kuishi na nini wafanye ili kuendeleza wilaya yao.

Wameeleza hayo wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii wilayani humo leo Februari 14, 2024  ikiwa ni siku tano tangu amefariki kiongozi huyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), mkoani Dar es Salaam.

“Tuna uchungu mkubwa, Lowassa alikuwa baba yetu, alikuwa akitulea, akituelekeza nini tufanye, tuishi vipi na tufanye nini ili wilaya yetu iendelee kuinuka,” amesema Laurent Frank.

Ameendelea kusema kuwa, Hayati Lowassa aliwahi kuwaita nyumbani kwake, na kuzungumza naye kuhusu kupata mikopo, ambapo walipata mikopo iliyowasaidia kufungua biashara mbalimbali.

“Mhe. Lowassa alitupatia mikopo hiyo ili tuinuke kiuchumi, ni kweli mikopo hiyo imewasaidia asilimia kubwa ya vijana kuinuka kiuchumi. Tunaendelea kumshukuru, kwani hakuna kiongozi aliyekuwa na msimamo ulio bora kama Mhe. Lowassa.

Kwa upande wake Devotha Gemuya ambaye ni fundi cherehani, amesema Hayati Lowassa amewajengea uwezo mabinti wa kimasai mpaka sasa wanaenda shule hawaolewi kama ilivyokuwa kipindi cha miaka ya nyuma.

“Mhe. Lowassa aliwezesha ujenzi wa shule nyingi za kata hapa Monduli, ambazo nyingi zilikuwa ni za bweni ili kuwanusuru watoto wa jamii ya kimasai na mila na desturi za kimasai.  Sasa hivi asilimia kubwa ya watoto wa kimasai wanaenda shule, na hata jamii ya kimasai imeelimika kupitia Mhe. Lowassa,” amesema Bi. D

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi