Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kuongezeka kwa Kina cha Maji ya Bahari Kwachangia Mmomonyoko wa Udongo na Upotevu wa Fukwe
Apr 05, 2024
Kuongezeka kwa Kina cha Maji ya Bahari Kwachangia Mmomonyoko wa Udongo na Upotevu wa Fukwe
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akijibu maswali bungeni jijini Dodoma leo Aprili 05, 2024.
Na Mwandishi Wetu

Kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari kumechangia mafuriko ya mara kwa mara yanayoukumba mkoa ya Pwani na hivyo kusababisha mmomonyoko wa udongo na upotevu wa fukwe.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameliarifu bunge jijini Dodoma leo Aprili 05, 2024 wakati akijibu swali la Mbunge wa Moshi Vijijini, Prof. Patrick Ndakidemi aliyehitaji kufahamu kama kuna ukweli kina cha maji ya Bahari ya Hindi nchini kimeongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi na nini athari zake.

 

Dkt. Jafo amesema kuwa kuongezeka kwa maji ya bahari kunasababishwa na kupanda kwa joto la dunia kutokana na kuendelea kuyeyuka kwa barafu katika maeno mbalimbali duniani. 

 

Amesema kuwa utafiti na vipimo vilivyopo maji ya Bahari ya Hindi katika pwani ya Dar es Salaam unaeleleza kuwa maji yanaongezeka kwa wastani wa kiasi cha milimita 6 kwa mwaka tangu mwaka 2002.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akibadilishana mawazo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma leo Aprili 05, 2024.

Kwa mujibu wa Waziri Jafo, upotevu wa bioanuwai muhimu ikiwemo mikoko na nyasi bahari ambavyo ni sehemu ya hifadhi ya mazingira ni miongoni mwa madhara ya kuongezeka kwa kina cha bahari.

 

Ametaja madhara mengine kuwa ni kupotea kwa ardhi na kuwaacha wananchi bila ya makazi na kushindwa kufanya shughuli za kilimo kutokana na changamoto na changamoto ya kuongezeka kwa kiwango cha bahari.

 

Waziri Dkt. Jafo ameongeza kuwa visima vya maji baridi mbali na kuingiwa na maji ya chumvi pia miundombinu ikiwemo barabara, gati za bandari na majengo hubomolewa na maji hayo.

 

Kwa upande mwingine Waziri Jafo amesema Serikali inaendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira kuzunguka mlima Kilimanjaro ili kulinda barafu isipate changamoto.

 

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Shally Raymond, Dkt. Jafo amepongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kuzalisha na kugawa miche kwa jamii ambayo inapandwa na kurejesha uoto wa asili.

 

 



 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi