Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kukamilika Soko la Kariakoo, Neema kwa Wafanyabiashara
Aug 26, 2023
Kukamilika Soko la  Kariakoo, Neema kwa Wafanyabiashara
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa akizungumza leo Agosti 26, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari uliolenga kueleza utekelezaji wa Serikali.
Na Na Mwandishi wetu

Ujenzi wa Jengo Jipya la  Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam kukamilika Oktoba mwaka huu na kutoa fursa kwa wafanyabiasha kufanya shughuli zao kwa masaa ishirini na nne.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa leo Agosti 26, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliolenga kueleza utekelezaji wa Serikali.

" Bilioni 28 zinatumika katika ujenzi wa jengo jipya la soko la Kariakoo litakalokuwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiasha 2,300 ikilinganishwa na 1,662 na tunatarajia kazi ya ujenzi wa jengo jipya na ukarabati wa jengo la zamani  zote zikamilike Oktoba 2023", alieleza, Bw. Msigwa.

Akieleza hatua iliyofikiwa katika ujenzi amesema jengo jipya limefikia asilimia 85 na ukarabati wa jengo la zamani asilimia 96.

Sanjari na ujenzi na ukarabati huo, Bw. Msigwa amesema Serikali inaimarisha miundombinu ya jiji la Dar es Salaam kwa kuwa ni eneo la kimkakati kiuchumi kwani linavutia wafanyabiasha kutoka mataifa mbalimbali hivyo kutoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi.

Miradi mingine inayotekelezwa katika jiji la Dar es Salaam ni pamoja na ule wa Mabasi yaendayo Haraka, Barabara za Lami, Elimu, 
Afya na Maji.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi