Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kuagwa kwa Mama Linah George Mwakyembe, Kunduchi Dar es Salaam
Jul 18, 2017
Na Msemaji Mkuu

Mwili wa marehemu mama Lina George Mwakyembe ukiwa umewasili nyumbani kwao Kunduchi Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa na ndugu pamoja na wanafamilia na kisha kupelekwa Kanisani kuombewa na kusafirishwa kwenda Mbeya.

Jeneza la marehemu mama Lina George Mwakyembe likiwa limebebwa mara baada ya kuwasili nyumbani kwao Kunduchi Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa na ndugu pamoja na wanafamilia na kisha kupelekwa Kanisani kuombewa na kusafirishwa kwenda Mbeya

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa ameinamia jeneza la mkewe mama Linah George Mwakyembe akiwa mwenye majonzi ya kuondokewa na mkewe wakati mwili ulipoletwa nyumbani kwake Kunduchi Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa akilia kwa uchungu mbele ya jeneza la mkewe mama Linah George Mwakyembe akiwa mwenyewakati mwili ulipoletwa nyumbani kwake Kunduchi Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwaamejumuika na viongozi mbalimbali, ndugu jamaa na marafiki kumuombea mke wake mama Linah George Mwakyembe katika Kanisa la K.K.K.T Kunduchi Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi