Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kopeni kwa Malengo ya Kujipatia Maendeleo - DAS Uyui
May 12, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_42971" align="aligncenter" width="900"] Katibu Tawala Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Moses Pesha (kulia) akimkabidhi jana Mkazi wa Kijiji cha Lutende Omary Mrisho (kushoto) hati miliki za kimila jana baada ya kupata mafunzo ya kujengewa uwezo ambayo yameandaliwa Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA).[/caption]

Na Tiganya  Vincent

SERIKALI ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora imewatahadharisha wakazi wa vijiji vya Miyenze na Lutende kutokopa fedha katika Taasisi za fedha bila malengo kwa ajili ya  kuepuka kunyang’anywa ardhi zao baada ya kushindwa kulipa madeni.

Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Uyui Moses Pesha  wakati wa kufunga mafunzo ya kujengewa uwezo wakulima  100 na viongozi 10 wa Kijiji cha Lutende na kukabidhiwa hati miliki za kimila.

Alisema Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) umeletea neema kwao ni vema wanapotaka kutumia hati zao kukopa iwe kwa kazi maalumu  na sio kukopa kopa ovyo ovyo bila kuwa na mipango mizuri ya kutumia fedha watakazokopeshwa kwa ajili ya kujiletea maendeleo.

“Hakikisheni mnapokopa iwe kwa ajili ya kazi maalumu na sio kwa ajili ya starehe , anasa na kununua mavazi na urembo…unapokopa hakikisha unalipa deni kwani usipolipa deni  hati hizo zitakuwa sio za kwenu tena hivyo mashamba yenu yatachukuliwa na Taasisi zilizowakopesha” alisema.

Pesha alisema sio vizuri mmoja wa wanafamilia akafanya siri wakati wa kwenda kukopa huku wenzake hawajui, kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha mgogoro baina yao na kufanya kuendelea kuisha kimasikini.

 Mkazi wa kijiji cha Lutende wilayani Uyui  Issa  Said Mtiliga akitoa neno la shukurani jana  kwa wakufunzi kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA)  kwa kuwajengea uwezo wakulima 100 waliopimiwa mashamba yao na kupata hati miliki za kimila ili waweze kutumia mtaji huo  kuboresha ufugaji wa mifugo ikiwemo kuku wa kienyeji.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala huyo wa Wilaya ya Uyui amewaonya wakazi wa Vijiji hivyo waliopatiwa hati miliki za kimila baada ya ardhi kupimwa kuepuka kuuza ovyo maeneo yao kwa kuwa wanaweza kusababu kuwa na maskini na kurudisha migogoro.

Alisema mwananchi anapotaka kuuza ardhi ni vema awe na sababu ya msingi na  pia katika kuuza lazima afuate taratibu na sharia zilizopo ili kuepuka kujiingiza katika umaskini.

Pesha aliongeza kuwa hata wanapouziana ni vema wafuate utaratibu wakati wa ubadilishani hati ili kuepuka migogoro baina ya mnununuzi na wanafamilia katika siku za baadae.

[caption id="attachment_42973" align="aligncenter" width="900"] Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu akitoa maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Katibu Tawala wa Wilaya ya Uyui kwa ajili ya kufunga mafunzo ya kujengewa uwezo wakulima 100 na viongozi 10 wa Kijiji cha Lutende na kukabidhiwa hati miliki za kimila jana.[/caption]

Naye Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu alisema mafunzo waliotoa kwa wakazi wa Kijiji cha Lutende na Miyenze katika Wilaya ya Uyui yamewajengea  uwezo wakulima wote waliopata hati ili waweze kutumia mtaji huo  kuboresha ufugaji wa mifugo ikiwemo kuku wa kienyeji.

Alisema pia wanapewa elimu ili waboreshe kilimo , utunzaji wa kumbukumbu za hesabu za kilimo na biashara na uandishi wa mpango wa biashara na uundaji wa vikundi vya uchumi kwa ajili ya uboreshaji wa uchumi wao na wilaya kwa ujumla.

[caption id="attachment_42975" align="aligncenter" width="900"] Katibu Tawala Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Moses Pesha akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima 100 na viongozi 10 wa Kijiji cha Lutende na kukabidhiwa hati miliki za kimila jana yaliyokuwayameandaliwa Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA).[/caption] [caption id="attachment_42976" align="aligncenter" width="900"] Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Lutende wilayani Uyui wakiwa katika mafunzo ya kuwajengea uwezo na kukabidhiwa hati miliki za kimila jana yaliyokuwayameandaliwa Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA).[/caption]  

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi