Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kongamano la Masuala ya Petroli Afrika Mashariki Kufanyika Kenya 2019
Dec 02, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_23957" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto), akishiriki katika Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ngazi ya Makatibu Wakuu na Wataalam, uliofanyika Kampala hivi karibuni. Pamoja naye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati) na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Gerson Mdemu.[/caption] [caption id="attachment_23958" align="aligncenter" width="988"] Mwakilishi kutoka Tanzania, ambaye ni Ofisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Steven Mbundi (kushoto), akisaini makubaliano ya masuala mbalimbali yaliyojadiliwa katika Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ngazi ya Makatibu Wakuu na Wataalam, uliofanyika Novemba 30 hadi Desemba 1, mwaka huu Kampala, sambamba na wenzake kutoka nchi nyingine za Jumuiya hiyo.[/caption]

Na: Veronica Simba - Kampala

Kongamano na Maonesho ya Tisa ya masuala ya Petroli kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, yanatarajiwa kufanyika nchini Kenya, Machi 2019.

Azimio hilo limepata baraka za Mkutano Ngazi ya Makatibu Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, uliofanyika Kampala, Desemba 1, mwaka huu.

Mkutano huo wa Makatibu Wakuu ni maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wenye lengo la kupitia nyaraka na taarifa za Maandalizi ya Mkutano wa Kazi wa Wakuu wa Nchi kabla ya kuziwasilisha kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi uliopangwa kufanyika mwezi Januari, 2018.

[caption id="attachment_23959" align="aligncenter" width="809"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto), akijadiliana jambo na Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Maendeleo ya Petroli, James Andilile (katikati) na Mhandisi Nishati, Samuel Mgweno, muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ngazi ya Makatibu Wakuu na Wataalam, uliofanyika Kampala Novemba 30 hadi Desemba 1, mwaka huu.[/caption] [caption id="attachment_23960" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya Ujumbe wa Wataalam kutoka Tanzania, wakiwa katika Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, uliofanyika Kampala, Novemba 30 hadi Desemba 1, mwaka huu.[/caption]

Kuteuliwa kwa Kenya kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo kubwa, kunatokana na mzunguko wa kawaida wa ratiba yake, ambapo makongamano yaliyotangulia yalifanyika katika nchi za Jumuiya husika kwa mlolongo wa Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi.

Hivyo basi, kutokana na mzunguko huo, Makatibu Wakuu wamebariki, Kongamano lijalo lifanyike Kenya kuanzia tarehe 6 hadi 8 Machi, 2019.

Aidha, Mkutano huo pia uliazimia kuwa, maandalizi ya Kongamano husika yaanze mapema ili kuwepo muda wa kutosha wa kujitangaza na kuvutia ushiriki wa mataifa mbalimbali duniani.

[caption id="attachment_23961" align="aligncenter" width="1017"] Meza Kuu – Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ngazi ya Makatibu Wakuu na Wataalam, uliofanyika Kampala, Novemba 30 hadi Desemba 1, mwaka huu.[/caption] [caption id="attachment_23962" align="aligncenter" width="750"] Wajumbe wa Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ngazi ya Makatibu Wakuu na Wataalam, uliofanyika Kampala, Novemba 30 hadi Desemba 1, mwaka huu, wakiendelea na Mkutano.[/caption]

Masuala mengine yahusuyo nishati, yaliyojadiliwa katika Mkutano huo ni pamoja na maendeleo ya upembuzi yakinifu kwa Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Kigali hadi Bujumbura, Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Mbarara – Mwanza - Isaka hadi Dar es Salaam, pamoja na kuoanisha mfumo wa kisheria na udhibiti wa masuala ya nishati.

Vilevile, Mkutano huo pia ulijadili maendeleo endelevu ya Kituo cha Ubora (Centre of Excellence) cha masuala ya Nishati Jadidifu na Matumizi Bora ya Nishati katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichopo kwenye Kitivo cha Uhandisi cha Chuo Kikuu cha Makerere, nchini Uganda.

Mbali na masuala ya nishati, sekta nyingine zilizojadiliwa katika Mkutano huo ni elimu ya juu, miundombinu, uchukuzi, fedha pamoja na afya.

Tanzania, kama ilivyokuwa kwa nchi nyingine wanachama, iliwakilishwa na wataalam mbalimbali kutoka sekta husika pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara hizo akiwamo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi