Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kilomita 39 za Barabara za Lami Zaanza Kujengwa Mji wa Serikali
Mar 23, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_51784" align="aligncenter" width="750"] Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshack Bandawe akionesha kazi ya ujenzi wa barabara za lami inavyoendelea[/caption]

Na Mwandishi Wetu

Ujenzi wa barabara za lami katika mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma waanza kwa kasi ili kuimarisha mawasiliano na huduma kwa wananchi.

Akizungumza leo Machi 20, 2020 katika mahojiano maalum, Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshack Bandawe amesema kuwa ujenzi huo unahusisha barabara zenye urefu wa kilomita 39 ndani ya mji huo.

[caption id="attachment_51785" align="aligncenter" width="750"] Eneo lililosafishwa tayari kwa ujenzi wa barabara za lami katika mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.[/caption]

“Serikali inaimarisha miundombinu ndani ya mji wa Serikali ikiwemo ujenzi wa barabara za njia mbili zenye urefu wa kilomita 28 na zenye njia 4 kilomita 11, ujenzi huu unaenda sambamba na kujengwa kwa miundombinu mingine kama TEHAMA, Afya, Makazi na Sehemu za Biashara”, Alisisitiza Bandawe

Akifafanua Bandawe amesema kuwa ujenzi wa miundombinu katika mji wa Serikali unaenda sambamba kujengwa kwa majengo ya gorofa kwa ajili ya matumizi ya Ofisi za Wizara 22.

Mji wa Serikali ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mwezi Machi 2019.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi